PSG HAWATAKI KUMUUZA NEYMAR KWA BARÇA BALI KWA REAL MADRID
Club ya PSG ya Ufaransa haina lengo la kumuuza Neymar kwa Barcelona, timu ambayo wafaransa hao hawana mahusiano nayo mazuri. Kwa hiyo, kwa mujibu wa 'Marça', PSG wameona bora mbrazili Neymar ni bora auzwe kwa Real Madrid huku wakiwa wameshawatangazia ofa karibu mara mbili. Lakini jibu la Madrid linaonekana ni 'Hapana!'
Madrid hawamtaki tena Neymar hata kama miezi kadhaa walionesha nia ya kuitaka saini yake. Neymar hatakiwi tena Barnabeu kwa sababu tayari wanaye Hazard, na pia wako na ndoto ya kumpata Mbappé. Kwa sasa Neymar atapaswa kusuniri PSG wamrahisishie kurudi Barcelona, maamuzi ambayo hayaonekani kuwa marahisi pamoja na namba 10 huyo na baba yake kuendelea kuwasumbua PSG ili aondoke.
Comments