Skip to main content

MANCHESTER UNITED WAWASAMBARATISHA WAGENI WAO CHELSEA FC WAWATANDIKA 4G OLD TRAFFORD

MANCHESTER UNITED WAWASAMBARATISHA WAGENI WAO CHELSEA FC WAWATANDIKA 4-0 OLD TRAFFORD


Manchester United jana waliwashangaza Chelsea baada ya kuwagawia kichapo cha magoli 4-0 kwenye uwanja wao wa nyumbani Old Trafford.

Mchezo wao huo ulikuwa ni wa ufunguzi kwao wa premier league ambao uliwakutanisha Ole Gunnar Solskjaer, aliyewahi kiwa mchezaji wa United miaka ya nyuma na sasa ni meneja wake na Frank Lampard naye aliwahi kuwa mchezaji wa Chelsea miaka ya hapo nyuma na sasa ni meneja wa the blues hao. 


Malejendari hawa walikuwa wakitazamwa na macho ya mashabiki wengi katika mechi hii ili kuona nani angemtambia mwenzake na hatimaye OGS akaibuka kifua mbele kwa ushindi huo mnono. 

Magoli ya Manchester United yalipachikwa na Marcus Rashford aliyefunga mawili, Anthony Martial akifunga moja na Daniel James, usajili mpya akifunga moja la nne.


Solskjaer aliwachezesha watatu ambao ni usajili mpya ambao ni Harry Maguire center back aliyesajiliwa kitoka club ya Leicester city, Aaron Wan-Bissaka beki wa pembeni aliyesajiliwa kutoka Crystal Palace na Daniel James aliyeingia baadaye aliyesajiliwa kitoka club ya Swansea city.


Comments

Popular posts from this blog

MAKUNDI CHAMPIONS LEAGUE NA SHIRIKISHO AFRIKA

Yanga Sc kundi A Klabu Bingwa Afrika na Simba Sc kundi A Shirikisho Afrika. Hapo chini ndio mpangilio wa makundi na timu zake. Je, nani kati ya timu zetu za bongo atatoboa kwenda robo fainali? Weka maoni yako kwenye komenti tafadhali.

Hawa Ndiyo Real Madrid Waliowafunga Man City Champions League Jana Usiku

Man City wakiwa wanaongo za kwa 2-1 dhidi ya Real Madrid huku zikiwa zimebaki dakika si zaidi  ya tatu walionekana kama ingekuwa ni timu ya tatu ya Uingereza kuifunga Madrid kwenye uwanja wa Bernabeu. Lakini vijana hao wa Mancini badala ya kuinza kampeni yao kwa ushindi walijikuta wakiachwa nyuma na kuwaangalia Madrid wakiibuka na ushindi baada ya Karim Benzema kusawazisha na kisha Cristiano Ronaldo kufunga goli la tatu na la ushindi, goli lililomfanya bosi wao Jose Mourinho kuslide uwanjani akishangilia goli hilo na Ronaldo. This was the real happiness now from Ronaldo BBC football pundit Robbie Savage alikuwa uwanjani huku Bernabeu. (quoting from BBC SPORTS) "Maicon was not at the races at all in the first half at right-back. He was a passenger and it was like City were playing with 10 men. Cristiano Ronaldo kept coming inside him. "In the second-half, Vincent Kompany looked at what was happening and came across to that wing more. Ronaldo did not...