Baada ya mwanaye kupata maambukizi ya corona virus, Freeman Mbowe anena haya:
Dear Chadema family! Baada ya Mwanangu Dudley kuwa positive na virusi vya Corona, familia nzima (Dar na Dodoma) iliingia kwenye “self isolation” kuondoa uwezekano wa kuambukiza wengine endapo tungekuwa na sisi tumeambukizwa. Habari njema ni kuwa wote tu salama na tumepata matokeo Negative!!
Poleni wote kwa hofu na asanteni sana wote kwa sala zenu! Indeed, ours, is an Amazing and Loving God.
Hata hivyo tutaendelea kuwa kwenye isolation hadi siku 14 zinazoshauriwa zitimie kamili.
Nawasihi wote tuendelee kuchukua tahadhari zote kwa kadiri na ushauri unaotolewa!!
Mbarikiwe sana!!
Freeman Aikaeli Mbowe
Comments