*GSM WAFANYA SUPRISE KWA WACHEZAJI WA YANGA*
Mdhamini wa Klabu ya Yanga leo alifanya Suprise ambayo wachezaji hawakuwa wameitarajia. Wachezaji wa Yanga waliitwa na Meneja wa Timu Abeid Mziba kuwa anaomba kukutana nao Mlimani City Bila kuwaambia anakusudia kufanya nini kwa wachezaji hao. Baada ya wachezaji kufika Mlimani City walipelekwa moja kwa moja kwenye Duka la GSM ndani ya Mlimani City na kukabidhiwa VOCHA YA SH. LAKI SITA KILA mchezaji na kutakiwa kutumia VOCHA hiyo kwenye maduka Ya GSM kwa kujipatia Bidhaa wanayoitaka. Wachezaji walifurahishwa sana na Jambo hilo. Nasasa GSM inakusudia kuwaalika wachezaji Waliooa kuwapeleka Wake zao kwa Suprise ambayo GSM hakuitanabahisha.
Wachezaji ambao wapo nje ya Dar watakutana na Vocha zao wakirejea.
Tazama picha Mbali mbali wakati wachezaji wa Yanga walipokuwa wakijipatia Mahitaji yao ndani ya Duka la GSM Mlimani City Leo 20/04/2020.
Comments