Skip to main content

UFAFANUZI KIFO CHA EVODIA KAPINGA, MUUGUZI, MUHIMBILI

UFAFANUZI KIFO CHA EVODIA KAPINGA MUUGUZI, MUHIMBILI.

Kuna taarifa inasambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Marehemu Evodia Kapinga amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Corona na kwamba alikua akihudumia wagonjwa wa Corona.

Marehemu Kapinga hajawahi kuhudumia wagonjwa wa wanaougua ugonjwa wa Corona

Marehemu alikua akitoa huduma kliniki ya watoto wenye tatizo la afya ya akili iliyopo jengo la watoto.

Marehemu ni mgonjwa wa siku nyingi aliyekua akisumbuliwa na MARADHI AMBAYO HATUWEZI KUYATAJA KULINGANA NA MAADILI YA TIBA.

Jana jumamosi tarehe 18 Aprili, 2020 saa NNE USIKU marehemu akiwa nyumbani kwake Kimara, alizidiwa ambapo watoto wake walifanya jitihada ya kumkimbiza Muhimbili lakini wakiwa njiani hali yake ilibadilika ndipo walipompeleka Hospitali ya karibu ya Sinza, Palestina.

Madaktari na Wauguzi walifanya kila jitihada kuokoa maisha yake bila mafanikio ambapo amefariki leo jumapili saa 09 alfajiri.

Hivyo, taarifa zinazosambaa kuwa kifo chake kinatokana na ugonjwa wa Corona siyo za kweli, ZIPUUZWE.

Imetolewa na;

Aminiel Aligaesha
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Comments

Popular posts from this blog

MAKUNDI CHAMPIONS LEAGUE NA SHIRIKISHO AFRIKA

Yanga Sc kundi A Klabu Bingwa Afrika na Simba Sc kundi A Shirikisho Afrika. Hapo chini ndio mpangilio wa makundi na timu zake. Je, nani kati ya timu zetu za bongo atatoboa kwenda robo fainali? Weka maoni yako kwenye komenti tafadhali.

Hawa Ndiyo Real Madrid Waliowafunga Man City Champions League Jana Usiku

Man City wakiwa wanaongo za kwa 2-1 dhidi ya Real Madrid huku zikiwa zimebaki dakika si zaidi  ya tatu walionekana kama ingekuwa ni timu ya tatu ya Uingereza kuifunga Madrid kwenye uwanja wa Bernabeu. Lakini vijana hao wa Mancini badala ya kuinza kampeni yao kwa ushindi walijikuta wakiachwa nyuma na kuwaangalia Madrid wakiibuka na ushindi baada ya Karim Benzema kusawazisha na kisha Cristiano Ronaldo kufunga goli la tatu na la ushindi, goli lililomfanya bosi wao Jose Mourinho kuslide uwanjani akishangilia goli hilo na Ronaldo. This was the real happiness now from Ronaldo BBC football pundit Robbie Savage alikuwa uwanjani huku Bernabeu. (quoting from BBC SPORTS) "Maicon was not at the races at all in the first half at right-back. He was a passenger and it was like City were playing with 10 men. Cristiano Ronaldo kept coming inside him. "In the second-half, Vincent Kompany looked at what was happening and came across to that wing more. Ronaldo did not...