Katika michezo iliyopigwa jana ya Mapinduzi Cup wababe wa soka Tanzania Simba na Yanga waligawa dozi muruwa na kuleta furaha na burudani kwa mashabiki wao.
Simba wakicheza mchezo wao majira ya saa 10 jioni waliwabamiza Selem View fc kwa 2-0 huku magoli yao yakifungwa na Sakho pamoja na Bwalya.
Yanga wakikipiga milango ya saa 2 na robo usiku wakawafurumusha timu ya Taifa Jang'ombe kwa 2-0 huku magoli yao yakipigwa na Heritier Makambo (mzee wa kuwajaza) pamoja na Denis Nkane the wonder Kid aliyesajiliwa akitokea Biashara United.
Timu zote za Kariakoo Dar es Salaam zilicheza zikiwakosa nyota wao kadhaa ambao huwa wanaanza kwenye kikosi cha kwanza lakini bado zilisalia zikiwa mwiba vile vile.
Comments