Yanga Sc kundi A Klabu Bingwa Afrika na Simba Sc kundi A Shirikisho Afrika. Hapo chini ndio mpangilio wa makundi na timu zake. Je, nani kati ya timu zetu za bongo atatoboa kwenda robo fainali? Weka maoni yako kwenye komenti tafadhali.
Shughuli itakuwa pale kwa Mkapa leo ikizikutanisha Yanga sc na Namungo kwenye mtanange wa NBC Premier League. Jana watani wa Yanga sc, Simba sc waliwalaza Singida Big Stars kwa 3-1 na mashabiki wao walifurahi sana. Leo ni zamu ya Wananchi kupata burudani huku wakitarajia kubaki kileleni kama ilivyo kawaida yao. Je Namungo watafungwa kirahisi? Wananchi mtafurahi leo? Tupe maoni yako kwenye comments.