Skip to main content

SPIKA AVUNJA KAMATI YA BUNGE

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda, jana aliivunja kamati ya bunge ya Niashati na Madini baada ya  kamati hiyo kutuhumiwa kuhusika na rushwa.

 Spika Anne Makinda

Wajumbe wa kamati hiyo wametuhumiwa na wabunge wenzao wiki hii kupokea rushwa toka kwa makampuni ya mafuta waliotaka wapewe tenda ya kusambaza mafuta kwa Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Makinda lifikia hatua ya kuvunja kamati hiyo baada ya mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa kumwomba kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa Makinda, kamati zote zinazotuhumiwa kwa mwenendo mbaya zitafanyiwa uchunguzi na zikikutwa na mmomonyoko wa maadili zitavunjwa na kisha kuhojiwa na tume ya maadili ya bunge chini ya mwenyekiti wake Bregadia Jenerali Mstaafu Hassan Ngwilizi.

Wajumbe wa kamati iliyovunjwa ni:-
Seleman Zedi (mwenyekiti), Diana Chilolo (mwenyekiti msaidizi), John Mnyika (Ubungo -Chadema), Yusuf Khamis (Nungwi- CUF), Mariam Kisangi (viti maalumu- CCM), Catherine Magige (viti maalumu- CCM), Abia Nyakabari (viti maalumu-CCM), Charles Mwijage (Muleba Kaskazini- CCM), naYusuf Nassir (Korogwe mjini- CCM).

Wengine ni:-
Christopher Ole-Sendeka (Simanjiro-CCM), Dr Festus Limbu (Magu mjini- CCM), Shaffin Sumar (Tabora Kaskazini-CCM), Lucy Mayenga (viti maalumu-CCM), Josephine Chagulla (viti maalumu- CCM), Mwanamrisho Abama (viti maalumu - Chadema), David Sillinde (), Suleiman Suleiman (Kishapu- CCM), Kisyeri Chambiri (Babati mjini-CCM), Munde Abudallah (viti maalumu - CCM), Sara Ally (viti maalumu-CCM), Vicky Kamata (viti maalumu- CCM), Mbarouk Ali (Wete-CUF), na Pamela Pallangyo (katibu).

Comments

Cornel Elikana said…
Wacha spika afanye hivo maana kila kukicha waoo wanaongeza vitambi huku mwananchi wa kijijini anahangaika

Popular posts from this blog

MAKUNDI CHAMPIONS LEAGUE NA SHIRIKISHO AFRIKA

Yanga Sc kundi A Klabu Bingwa Afrika na Simba Sc kundi A Shirikisho Afrika. Hapo chini ndio mpangilio wa makundi na timu zake. Je, nani kati ya timu zetu za bongo atatoboa kwenda robo fainali? Weka maoni yako kwenye komenti tafadhali.

Hawa Ndiyo Real Madrid Waliowafunga Man City Champions League Jana Usiku

Man City wakiwa wanaongo za kwa 2-1 dhidi ya Real Madrid huku zikiwa zimebaki dakika si zaidi  ya tatu walionekana kama ingekuwa ni timu ya tatu ya Uingereza kuifunga Madrid kwenye uwanja wa Bernabeu. Lakini vijana hao wa Mancini badala ya kuinza kampeni yao kwa ushindi walijikuta wakiachwa nyuma na kuwaangalia Madrid wakiibuka na ushindi baada ya Karim Benzema kusawazisha na kisha Cristiano Ronaldo kufunga goli la tatu na la ushindi, goli lililomfanya bosi wao Jose Mourinho kuslide uwanjani akishangilia goli hilo na Ronaldo. This was the real happiness now from Ronaldo BBC football pundit Robbie Savage alikuwa uwanjani huku Bernabeu. (quoting from BBC SPORTS) "Maicon was not at the races at all in the first half at right-back. He was a passenger and it was like City were playing with 10 men. Cristiano Ronaldo kept coming inside him. "In the second-half, Vincent Kompany looked at what was happening and came across to that wing more. Ronaldo did not...