Kwa mara nyingine tena Mashetani wekundu toka jiji la Manchester wameshindwa kutamba leo katika mechi yao wakiwa ugenini dhidi ya Barnley baada ya kulazimisha gari sare tasa yaani bila bila.
Kila mtu alidhani United wangepata ushindi wao wa kwanza katika ligi. Lakini pamoja na kujaribu sana kuutawala mchezo bado safu ya ushambuliaji ilibaki kuwa butu. Safu hiyo ikiongozwa na Van Persie, Rooney, Mata na Di Maria ilishindwa kabisa kabisa kufikisha mpira kwenye nyavu ya wapinzani wao.
Di Maria alijaribu sana kuonesh makeke hasa ale alipotoa Pande safi sana kwa Van Persie ambaye aliachia shuti safi lakini lilikataliwa na kipa wa Barnley.
Valencia ndiye mchezaji aliyepata mipara Mingi sana lakini alikosa ubunifu wa kupiga krosi au kuto assist ambazo zingezaa matuda.
Young naye vilevile hapo alijaribu kupenya Mara kadhaa lakini pia ubunifu haukuwa kichwani mwake.
Rooney na Van Persie walionekana wazito sana kwenye kufanya maamuzi na kuwa wachezaji wa kawaida na wenye kukabika kiurahisi sana.
Ni Barnley ndo waliofanya mashambulizi ya hatari huku shuti moja likigonga mwamba wa juu na lingine likipangulia na kipa De Gea.
Evans ni beki ambaye alikuwa na makosa mengi sana katika safu ya ulinzi. Kidogo aigharimu timu yake pale aliporudisha mpira dhaifu kwa De Gea ambao kidogo unaswe na adui lakini umahiri wa De Gea aliyetokea haraka na kuklia hatari ile.
United walikuwa wapate penati katika kipindi cha pili baada ya shuti LA Young kutua mikononi kwa beki wa Barnley lakini refa aligoma kutoa penati.
Januzay, Anderson na Welbeck waliingia baada ya Van Gaal kuwatoa Van Persie, Di Maria.
Nini mwisho wa United kwenye huu msimu?
Comments