Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2016

Madiwani Mbeya vijijini wagoma kununua suti ya mwanasheria wa Halmashauri.

Manchester City wamekumbwa na nini?

Jana kulipigwa mtanange  wa FA CUP katika dimba la Stanford Bridge kati ya Chelsea na Man City. mchezo ulianza kwa kawaida sana na hata kuwafanya mashabiki kudhani kuwa wasingefurahia kabisa. Lakini mambo yalianza kubadilika baada ya Chelsea kuanza kuongoza baada ya kutupia goli katika kipindi cha kwanza goli ambalo baada ya muda mfupi sana lilisawasishwa na wapinzani wao Man City. Kipindi cha pili kilianza kwa majanga kuangukia upande wa vijana wa Manuel Pelegrin ambao walikuwa wametembelea darajani hapo. Magoli yalianza kumiminwa ukiachia lile la Costa mengine yalifungwa na Willian, Hazard, Traore na Cahil. Wengi wanajiuliza swali hili... "Kipigo hicho toka kwa Chelsea ni kufuatia ujio wa Pep msimu unao, kwamba Manuel anafanya makusudi? kwani kikosi alichopanga kilijaa makinda wengi sana na hata golikipa alionekana kukosa uzoefu kabisa.. Je, Manuel kajiondoa makusudi ili afokasi kwenye ligi na champions? 

Hizi hapa picha 28 za mtanange wa jana kati ya Yanga na Simba. Furahia Mtu wangu

Photos Via MICHUZI BLOG

LIGI KUU BARA YAWA SHUBIRI KWA WANA MSIMBAZI

Baada ya kusubiri miezi, wiki, siku na hata saa hadi dakika hatimaye wakati ulitimia pale ulipotokea mtanange mkali wa kukata na shoka kama sio mundu kati ya watani ama maadui wa jadi katika soka la bongo, Yanga na Simba, mchezo uliopigwa kwenye dimba la taifa huku ukitawaliwa na mbwembwe, fitina na majigambo toka kwa mashabiki wa pande zote mbili. Mchezo ambao tumeshuhudia wana Jangwani Dar Young Africans wakiwazodoa watani wao alimaarufu wekundu wa msimbazi kwa kuwachapa magoli mawili moja katika kila kipindi cha mchezo huo. Alikuwa ni Donald Ngoma aliyewainia mashabiki wa jangwani kwa kupachika bao baada ya kuunasa mpira uliopigwa na mabeki wa Simba wakirudisha pasi nyumba, ndipo akawalamba chenga beki na kipa wake na kuukwamisha wavuni. Simba walijaribu kwa nguvu zote kurudi mchezoni na kufanikiwa kushambulia mara kadhaa lakini hadi kipindi cha kwanza kinaisha Yanga 1-0 Simba. Kipindi cha pili nacho kilianza kwa kasi huku kila timu ikipanga mashambilizi lakini walionekana ni Ya...