HIVI PUNDE : PAUL MAKONDA AZUIA AGIZO LA KUONDOA TINT KWENYE MAGARI Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda amewaagiza Polisi jijini Dar kusitisha utekelezaji wa amri inayowataka wananchi wenye magari kuondoa tint kwenye vioo vya magari yao. Agizo hili ambalo hapo awali utekelezaji wake ilikuwa uanze kesho, Paul Makonda amesema litawaletea usumbufu wananchi kwani sababu za utekelezaji wake hazina mashiko. "Tafsiri yake ya kwanza ambayo agizo hilo inapeleka kwenye jamii ni kuwa wenye tinted kwenye vioo vya magari yao, kama sio wao basi wanaoyatumia, ni wahalifu. Jambo ambalo si kweli kwani yapo magari yanakuja yakiwa na vioo tinted, pia wengine wanaitumia tinted kama njia ya kujilinda dhidi ya watu wabaya hasa wakinamama," amesema Paul Makonda. "Aidha, mkoa wa Dar Es Salaam sio kisiwa, kuna watu wanaingia kila siku; Je, magari yao tu nataka wayapaki Chalinze?" ameuliza kwa mshangao Paul Makonda. Paul Makonda amehitimisha kwa kuwataka Polisi kutafuta njia sa...
Brings You Global News!