Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2017

Lazaro Nyalandu Ahama CCM na Kujiuzulu Ubunge.

Lazaro Nyalandu Ameyasema haya, NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa. AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA. VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania ...

Diamond Platnumz becomes first African Artist to Platinum

Joti naye auaga ukapera

Msanii wa maigizo ya vichekesho nchini maarufu kama Joti nae ameliaga kundi la makapera baada ya kufunga ndoa. Msanii Joti pia ni maarufu sana katika matangazo ya mtandao wa Tigo. Joti pia ni maarufu sana katika kuigiza sehemu mbalimbali kwani mara nyingi huigiza kama kijana wa kawaida, babu, mtoto na wakati mwingine huigiza kama msichana. Hongera sana Joti kwa kuoa! May your marriage last forever!

Manchester United Walinda Heshima Nyumbani. United 1, Spurs 0

Goli lilipigwa na super sub Anthony Martial lilitosha jana kuipa Manchester United ushindi katika dimba la nyumbani Old Trafford na kuwanyamazisha kabisa Totten Ham Spurs na mashabiki wao. Spurs wako kwenyw form ya hali ya juu na inashikilia nafasi ya tatu kwenye masimamo wa ligi hiyo ya EPL nyuma ya United na vinara wakiwa ni Manchester City. Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, timu zote mbili zilicheza vizuri na kuwa na kosakosa za hapa na pale hasa Man United ambao walionekana wenye ari ya ushindi hasa ikizingatiwa walikuwa nyumbani. Wengi walitarajia kwamba United wangepaki basi kama walivyofanya nyumbani kwa Liverpool ama kupoteza mchezo huo kama ilivyotokea nyumbani kwa Huddersfield, lakini matarajio yao hayo yaliyoyoma na kushuhudia Manager wa United José Mourihno akimtoa Marcus Rashford na kumwingiza Anthony Martial ambaye baada ya muda alipokea pande toka kwa Romelu Lukaku aliyempasia kwa kichwa (assist) naye bila ajizi aliwatoka mabeki wa Spurs na kuupeleka m...