LIONEL MESSI AWATAKA BARCELONA WAMSAJILI MARCOS ALONSO WA CHELSEA FC
Baada ya mechi ya Barcelona vs Chelsea kwenye 2nd leg mechi ambayo FC Barcelona waliwatwanga the Blues 3-0, Lionel Messi ameibuka na kudai kuwa alivutiwa sana na ukabaji wa beki wa Chelsea Marcos Alonso ingawaje aliwanyanyasa na kupachika magoli mawili peke yake. Sasa baada ya kuvutiwa na beki huyu ameamua kuchukua hatua na kuwaomba wakubwa wake kumsajili Alonso ili kuimarisha eneo la ulinzi kwa timu yake huku ikijulikana kwamba Messi anatarajiwa kuukwaa ukepteni pale Andrés Iniesta atakapostaafu.
Marcos Alonso amejizolea sifa na umaarufu wa kutosha kwani amekuwa beki imara asietikiswa ovyo ovyo. Pia amekuwa mpiga free kick mzuri sana mwenye kupachika magoli ya mtindo huo.
Huyu beki Marcos Alonso hata ningekuwa mimi ni kocha ningemsajili.
Comments