MAN UNITED 2-1 ARSENAL. WENGER APIGIWA MAKOFI YA BYEBYE NA MASHABIKI WA UNITED. FERGUSON AMKABIDHI ZAWADI WENGER HUKU MOURINHO AKIWA MTULIVU AKISHUHUDIA.
Manchester United 2-1 Arsenal
Marouane Fellaini anafungwa kwa kichwa dakika za majeruhi 90+1 na kuwapatia United goli la pili na la ushindi baada ya Henrikh Mkhitaryan kusawazisha goli la Paul Pogba.
-Konstantinos Mavropanos anacheza kwa mara ya kwanza mechi yake ya premier league akiwa Arsenal.
-Paul Pogba anafunga goli la kwqnza katika kipindi cha kwanza baada ya Alexis Sanchez kupiga kichwa na mpira kugonga mwamba na kurudi.
-Romelu Lukaku alilazimika kutoka baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Marcus Rashford mapema kipindi cha kwanza.
-Dakika 6 baadae kipindi cha pili Mkhitaryan anasawazisha goli dhidi ya timu yake ya zamani.
-Rashford anafunga goli lakini linakataliwa kwa kuwa ni offside.
-Na hatimaye Sub Marouane Fellaini anavunja upinzani wa vijana wa Wenga na kuipatia ushindi United kwa kufunga kwa kichwa goli la pili.
Comments