Fifa World Cup 2018. Mechi za Kwanza. Ronaldo Acheka, Messi Anuna
Tuziangalie mechi za ufunguzi, yaani mechi za kwanza kwa kika timu ama nchi kwenye mashindano ya fainali za kombe la dunia 2018 kule Urusi lakini hasa kwa mataifa mawili wanayotokea mastaa ama wapinzani wakubwa wawili ambao wanacheza kwenye La Liga kule Hispania, namaanisha Mreno Cristiano Ronaldo na Muajentina Lionel Messi.
Katika mechi yao Ureno ama Portugal vs Spain, Ronaldo aliibuka shujaa baada ya yeye na wenzake kulazimishana droo ya 3-3 dhidi ya Hispania huku Ronaldo akiweka rekodi nyingine, akifunga hat trick yaani mabao matatu ndani ya mechi moja, kwa penati, shutu la mbali pamoja na free kick.
Ronaldo akishangilia goli
Kwa upande wa hasimu wake mkubwa Lionel Messi, yeye leo ameshindwa kabisa kufurukuta wakati taifa lake Argentina walipovaana na Iceland. Akipiga mashuti 11 hakufanikiwa kabisa kutikisa nyavu za Iceland kwani hata goli lao lilifungwa na Aguero. Huku akipata nafasi sawa na Ronaldo, yaani penati pamoja na Free kick yenye umbali unaofanana na ile ya Ronaldo lakini akakosa vyote. Hakufunga penati, hakufunga free kick na wala yale mashuti yake hayakulenga lango wala kumsumbua kipa wa Iceland.
Messi akijiinamia asijue nini amefanya
Ebu tusubiri tuone yajayo katika mechi za zinazofwata. Je Ronaldo ataendela na makeke yake ama atapoa? Na je Messi atainua nyoyo za mashabiki wake na kufanya mambo makubwa kwa taifa lake ama ataendelea kupoa?
Ronaldo akishangilia goli
Comments