EPL: CHELSEA 3, ARSENAL 2
- Chelsea wamewapiga Arsenal kwenye London Derby leo usiku huku Marcos Alonso akifunga goli la ushindi.
- Pedro alikuwa wa kwanza kuzichungulia nyavu za Arsenal baada ya dakika Tisa tu akipokea cross ya Alonso.
- Pierre-Emerick Aubameyang akikosa goli la wazi na rahisi la kusawazisha kabla ya Alvaro Morata kuongeza la pili kwa Chelsea.
- Henrikh Mkhitaryan akafunga goli la kwanza kwa Arasenal kuto!ea ndani ya box, huku Alex Iwobi akifunga la pili na KUWEKA mambo sawasawa yaani 2-2.
- Alonso akipata msaada mkubwa toka kwa Hazard akamaliza kazi kwa kuoiga goli la tatu na la ushindi kwa Chelsea na kuwafanya Arsenal wamalize mchezo wa pili wa Epl bila pointi.
Comments