EPL SIDE: MAN UNITED WALA KISAGO TOKA KWA BRIGHTON. FT: BRIGHTON 3, MAN UNITED 2
Kikosi cha José Mourinho kimepokea kichapo kikali toka kwa Brighton katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa Epl uliopigwa leo jioni.
- Glenn Murray akifungua akaunti ya ambao kwa Brighton & Hove Albion FC akimalizia kwa ustadi sana na kumwacha De Gea asijue la kufanya.
- Seagulls akaongeza la pili na kuwafanya United wazidi kuchanganyikiwa kama sio kujichanganya.
- Manchester United wakapata bao la kwanza kupitia Romelu Lukaku kwa kichwa baada ya kazi nzuri ya Luke Shaw.
- Lakini muda mfupi kabla ya Half time Eric Bailly akagawa penati kwa wenyeji wao na ikafungwa na Pascal Gross na kufanya kuwa 3-1.
- Paul Pogba akaifungia United goli la pili kwa mkwaju wa penati baada ya Fellaini kuchezewa ndivyo sivyo eneo la Hatari. Lakini haikusaidia chochote kwa United Kwani huo ndio ukawa mwisho wa mchezo.
Comments