LA LIGA: BARCELONA 3, ALAVES 0. Ni Zamu ya Philippe Coutinho na Lionel Messi
- Inaanza na Lionel Messi kugonga mwamba wa juu huku kipindi cha kwanza kikiyoyoma kwenye mchezo wa La Liga Jana Jumamosi jioni.
- Ndipo Barcelona wakamwingiza Philippe Coutinho aliyekiwa bench mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika tasa.
- Ndipo Lionel Messi akavunja ukimya katika dakika ya 64 kwa kufunga goli kwa shuti la free kick under the wall.
- Coutinho naye akaja na kuongeza la pili dakika saba baadaye akiupachika mpira kwenye kona ya mbali kule anakotagia sio kuku tena bali kanga kama ilivyo kawaida yake. (Sijui kwa nini Liverpool walimuuza)
- Messi akarudi tena kwenye nyavu za Alaves na kufunga la pili na la tatu kwa Barcelona katika dakika ya lala salama kabisa na kupeleka ushindi mnono Nou Camp.
Comments