Hivi sasa baadhi ya marais wa nchi mbalimbali wameanza kusifia jihudi, maarifa na kasi ya rais wa awamu ya tano ya Tanzania Dr. John Pombe Magufuli. JPM tangu aingie madarakani takribani mwezi mmoja amekuwa akifanya juhudi za dhati za kuikomboa nchi toka kwa mapapa ya ufusadi akianzia wizara ya fedha, bandari, TRA na sehemu nyingine akiwawajibisha wala rushwa, wakwepa kodi na wahujumu uchumi wa nchi huku wengine vibarua vyao vikiota nyasi na wengine hata kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka. JPM alionekana leo ktk mtaa wa feri DSM akifanya usafi na majirani zake akitii amri aliyoitangaza mwenyewe ya kuwa maadhimisho ya uhuru wa Tanganyika ya 9 Disemba yasiwe na sherehe na badala yake siku hiyo iadhimishwe kwa kufanya usafi ili kutokomeza magonjwa yanayolitia taifa aibu hususan kipindupindu. Watanzania wengi kila mji wametii amri kwa furaha na kutoka tangu asubuhi wakifanya usafi. Wengi wameonekana kufurahia uamuzi wa mh JPM wa kutokuwa na sherehe za uhuru na kuifanya serikali kutunz...