MANCHESTER UNITED vs CHELSEA FC LEO #EPL USIKOSE NA USIKUBALI KUSIMULIWA #TheBattleAtOldTrafford: Jioni ya leo miamba ya kabumbu la Uingereza inakutana katika mpambano unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua. Manchester United leo wanawakaribisha mahasimu wao Chelsea pale Old Trafford kwenye mchezo wa round ya pili ya Premier League. Ikumbukwe kuwa Katika mchezo wa kwanza walipokutana pale Stamford Bridge Chelsea waliwanyuka Man United 1-0, goli lililofungwa na Alvaro Morata kwa kichwa. Kuna kama kauadui flani hivi kati ya makocha Antonio Conte wa Chelsea na José Mourinho wa Man United. Na huu ni uhasimu ambao kila mmoja wao anajaribu kuuficha na kuonesha kuwa hawana shida kati yao. Mourinho amenena kuwa game kati ya timu hizi mbili ni ya kawaida kwake kama game nyingine nyingine na hakuna chochote special kuihusu. Lukaku, Rashford, Martial, Matic, Pogba, De Gea na wengineo wanategemewa kuongoza kikosi cha man United leo huku Morata, Fabregas, Pe...