Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2018

London Derby: EPL: SARRIBALL YADODA WEMBLEY

#LondonDerby: #Epl: #Sarriball style yadoda Wembley! Tottenham 3-1 Chelsea: Magoli ya Dele Alli,  Harry Kane na Son yaharibu mpango wa Chelsea wa kutofungwa! Kutofungwa kwa Chelsea katika epl kumeingia doa baya lisilotakata hata kwa sabuni gani baada ya mchezo mzuri wa kuvutia wa Tottenham katika dimba la Wembley uliohakikisha mashabiki wa Chelsea wanalizwa machozi ya damu kwa kuwekwa magoli mara 3.  Dele Alli akifungua ukurasa wa magoli kwa wenyeji baada ya dakika 7 tu za mchezo huku kichwa chake kikipeleka mpira kwenye post ya mbali sana,  aka anakotagia kanga.  Harry Kane akaongeza la pili akiichungulia kona ya chini baada ya mabeki wa Chelsea kumwachia apige shuti la mbali. Son akafanya magoli kuwa 3 kwa Spurs mapema kunako kipindi cha pili baada ya mkorea huyo kufanya kitu kinaitwa kwa kizungu sensational solo goal.  Olivier Giroud akaingia kutokea bench na kufunga goli la kufutia machozi kwa wageni Chelsea.

Huyu Hapa Ndiye Mchezaji Bora wa Mwaka Sweden

Victor Lindelof

Santiago Solari Kuwa Kocha Mkuu wa Real Madrid

Klabu ya Real Madrid inatarajia kumtangaza Santiago Solari kuwa kocha wa klabu hiyo mpaka mwisho wa msimu huu baada ya kuiongoza Madrid kwenye michezo minne akiwa kama kocha msaidizi. Solari ameshinda michezo yote minne aliyoiongoza Real Madrid na kufanya raisi wa Real Madrid Florentino Perez kumwamini na kumpa kazi hiyo. Awali  Real Madrid walitaka kumpa nafasi hiyo kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte lakini dili hilo lilivunjika hatua za mwisho baada ya kushindwa kuelewana huku Conte akidai sababu ni kwamba alitaka kuchukua timu mwezi June na sio katikati ya msimu. Source: #kwetusport

Liverpool Wachezea Kichapo huku Barcelona wakibanwa Mbavu na Inter katika UCL

Wakati Liverpool wakichezea kichapo cha 2-0,  Spurs wafufua matumaini ya kuendelea na UCL na Barcelona wakibanwa mbavu na Inter,  Dortmund nao walazwa ugenini na Monaco wakishangazwa mbele ya Club Brugge. Hatari tupu!