Skip to main content

Posts

Showing posts from March, 2020

Polisi zaidi ya 700 wapata covid-19 New York

Polisi zaidi ya 700 mjini New York wamepata CoronaVirus, inaripotiwa wengi wamepta wakati wakitimiza majukumu yao mitaani wakati wa Karantini fupi huko mjini New York. New York Police Department (NYPD) inaripoti kuwa asilimia 12 ya askari wake wako nyumbani wanaumwa. New York ndio mji ulioathirika zaidi na CoronaVirus nchini Marekani, New York mpaka sasa inakesi 664,071 za Covid-19. #SamMisagoTV

Mkurugenzi wa Takukuru Athibitishwa na Rais Magufuli

#DODOMA :- KAIMU MKURUGENZI TAKUKURU ATHIBITISHWA NA RAIS MAGUFULI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amthibitisha Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) Brig. Jenerali John Mbungo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo baada ya kuokoa Shilingi Bilioni 8.8 za wakulima. Rais Dkt. Maguguli Amechukua uamuzi huo baada ya kupokea ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) na ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mapema leo katika Ikulu ya Chamwino Jijini, Dodoma. #CCMAmaniyaTanzania

Meya wa Iringa Ang'olewa kwa kura 14

MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA IRINGA ANG’OLEWA MADARAKANI  Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani Manispaa ya #Iringa umetanga kumuondoa madarakani Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo #AlexKimbe, huku mwenyewe akisema mchakato huo haujafata taratibu hivyo ataendela kuwa Meya wa Manispaa hiyo. Mkutano huo uliokuwa na wajumbe 26 uliamua kupiga kura. Kati ya kuta 26 zilizopigwa kura 12 zikiharibika na kura 14 zikipiga kura ya ndio kumtaka meya huyo aondoke madarakani. #AzamTVUpdates

ZANZIBAR YATHIBITISHA MGONJWA MWINGINE WA CORONA

#BreakingNews ZANZIBAR YATHIBITISHA MGONJWA MWINGINE WA CORONA Zanzibar yathibitisha mgonjwa wa tatu wa COVID-19 na kufanya idadi ya waambukizwa Tanzania kufikia 14. Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid Hamad amethibitisha. Mgonjwa huyo mwanamke raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 57 alirejea nchini akitoka uingereza na shirika la ndege la Qatar na kuifanya Zanzibar kuwa na idadi ya wagonjwa watatu wenye mambukizi ya virusi vya corona. #CoronaDuniani #CoronaKenya #CoronaUchumi #CoronaTanzania #CoronavirusPandemic Credit: #AzamTv

Kikongwe wa miaka 102 apona corona virus Genoa, Italia

#ITVUPDATES:Italica Grondona mwanamke mwenye miaka 102 amepona ugonjwa wa Corona baada ya kukaa hospitali mjini Genoa nchini Italia kwa zaidi ya siku ishirini. #ItvTanzania #CNN

Baada ya mwanaye kupata maambukizi ya vorona virus, Mbowe anena haya

Baada ya mwanaye kupata maambukizi ya corona virus, Freeman Mbowe anena haya:  Dear Chadema family! Baada ya Mwanangu Dudley kuwa positive na virusi vya Corona, familia nzima (Dar na Dodoma) iliingia kwenye “self isolation” kuondoa uwezekano wa kuambukiza wengine endapo tungekuwa na sisi tumeambukizwa. Habari njema ni kuwa wote tu salama na tumepata matokeo Negative!! Poleni wote kwa hofu na asanteni sana wote kwa sala zenu! Indeed, ours, is an Amazing and Loving God. Hata hivyo tutaendelea kuwa kwenye isolation hadi siku 14 zinazoshauriwa zitimie kamili. Nawasihi wote tuendelee kuchukua tahadhari zote kwa kadiri na ushauri unaotolewa!! Mbarikiwe sana!! Freeman Aikaeli Mbowe Credit: #ChademaBreakingNews

Visa vya maambukizi ya covid-19 Kenya

Kenya imethibitisha visa vingine 7 vya maambukizi ya virusi vya Corona na kufikisha idadi ya wagonjwa kuwa 38. Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema kuwa katika wagonjwa hao, wanne ni wakenya, wawili ni raia wa Congo na raia mmoja ni wa China. Credit: #ItvTanzania

Wenzetu Kenya wamefikia hatua hii. Sisi tushukuru serikali yetu viongozi wanajitambua

Huu ni mpango madhubuti wa kuzuia kutembea ovyo kufuatia serikali kutoa tamko hilo ili kupambana na maambukizi ya corona virus aka Covid-19. Na hawa kwenye picha ni baadhi ya wananchi wlaiowekwa chini ya ulinzi kwa kosa la kukaidi amri hiyo huko Kenya.  Swali ni kwamba, kama kwenye kundi hilo wapo walioambukizwa na wasioanbukizwa, watapona kweli? Tuombe sana rehema za mwenyezi Mungu juu yetu.

Je, ni kweli Meya wa Iringa aliwahi kupewa pesa hizi akazikataa?

MEYA WA IRINGA MJINI ANASTAHILI HESHIMA KUBWA. 2016 Alipewa Million 150 akazitosa,  2017 akapewa 180 akazitosa ,  2019 Walimletea milion 200, 250 na 300. Mara Tatu, Akazitosa.  Leo anaingia Chumba cha kuvaa Ameletewa Milion 400 amewatosa.