Skip to main content

Posts

WAGONJWA 37 WAPONA CORONA, 71 WASUBIRI VIPIMO VYA MWISHO

WAGONJWA 37 WAPONA CORONA, 71 WASUBIRI VIPIMO VYA MWISHO Wagonjwa 37 waliokuwa wameambukizwa virusi vya Corona #COVID19 wamepona na kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya vipimo vya mwisho kuthibitisha kwamba hawana maambukizi. “Watu hawa 108 hawana dalili zozote za ugonjwa kama vile homa au mwili kuchoka isipokuwa wapo katika vituo vya matibabu kusubiri vipimo vya mwisho ili kuthibika kwamba hawana virusi vya corona kabla ya kuruhusiwa kutoka vituoni,” amesema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. Waziri Ummy Mwalimu amewataka watu waliopona ugonjwa huo kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya ili kujikinga na maambukizi mapya ya COVID-19 kwani zipo tafiti zilizofanyika nchi mbalimbali ikiwamo China zimeonyesha kuwa watu wanaweza kupata maambukizi mapya kama asilimia 14. “Tunapenda kuwahimiza watu waliopona watoe elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) kwa jamii. Pia, Nitumie fursa hii kwa niaba ya Serikali kutoa shukrani ...

*GSM WAFANYA SURPRISE KWA WACHEZAJI WA YANGA*

*GSM WAFANYA SUPRISE KWA WACHEZAJI WA YANGA* Mdhamini wa Klabu ya Yanga leo alifanya Suprise ambayo wachezaji hawakuwa wameitarajia. Wachezaji wa Yanga waliitwa na Meneja wa Timu Abeid Mziba kuwa anaomba kukutana nao Mlimani City Bila kuwaambia anakusudia kufanya nini kwa wachezaji hao. Baada ya wachezaji kufika Mlimani City walipelekwa moja kwa moja kwenye Duka la GSM ndani ya Mlimani City na kukabidhiwa VOCHA YA SH. LAKI SITA KILA mchezaji na kutakiwa kutumia VOCHA hiyo kwenye maduka Ya GSM kwa kujipatia Bidhaa wanayoitaka. Wachezaji walifurahishwa sana na Jambo hilo. Nasasa GSM inakusudia kuwaalika wachezaji Waliooa kuwapeleka Wake zao kwa Suprise ambayo GSM hakuitanabahisha. Wachezaji ambao wapo nje ya Dar watakutana na Vocha zao wakirejea. Tazama picha Mbali mbali wakati wachezaji wa Yanga walipokuwa wakijipatia Mahitaji yao ndani ya Duka la GSM Mlimani City Leo 20/04/2020. @bigbros_tanzania_tv

Tundu Lisu amtaka Rais kurudi Ikulu

Tundu Lisu amtaka Rais kurudi Ikulu 'Mheshimiwa Rais Magufuli, Ikulu ya nchi yetu haiko Chato. Ikulu iko Dar es Salaam na Dodoma. Toka mafichoni Chato uje Ikulu kuongoza nchi dhidi ya corona. Ndivyo wanavyofanya viongozi wenzako dunia nzima. Usiwaachie Ummy na Majaliwa jukumu hilo. Wewe ndiye Rais, sio wao.'- Tundu Lissu @Tundulisu Chanzo: @kwanzatv

BREAKING NEWS: WAGONJWA WAPYA 84 WA CORONA TANZANIA

BREAKING NEWS: WAGONJWA WAPYA 84 WA CORONA TANZANIA Waziri Ummy Mwalimu ametangaza wagonjwa wapya 84 wa Corona nchini Tanzania, jumla wamefikia wagonjwa 254. DSM -33 Arusha -4 Mbeya -3 Kilimanjaro-3 Pwani -3 Tanga-3 Manyara-2 Tabora -1 Dodoma -3 Ruvuma -2 Moro- 2 Lindi-1 Mara-1 Mwanza -3 Mtwara -1 Kagera-1 Rukwa-2 Zanzibar-16 @eatv_tz

#COVID-19: TAARIFA KUTOKA BUNGENI, MBUNGE MMOJA AMEAMBUKIZWA CORONA

"Tumepata taarifa kuwa mmoja wetu amepata maambukizi ya #COVIDー19. Mgonjwa huyo anaendelea vizuri na serikali inaendelea kumuangalia na kumpatia matibabu stahiki, na maelezo ya mbunge huyo alisafiri kwenda Dar es Salaam siku za hivi karibuni."- Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson @swahilitimes

PIERRE LIQUID ATHIBITIKA KUWA NA COVID-19

CORONAVIRUS-TANZANIA: PIERRE LIQUID ATHIBITIKA KUWA NA #COVID19 - Peter Mollel maarufu Pierre Liquid sasa yupo Hospitali ya Amana akiendelea na matibabu - Amesema anahisi amepata #CoronaVirus baa maana ndio maeneo yake ya kujidai @jforum #JFCOVID19_Updates

UFAFANUZI KIFO CHA EVODIA KAPINGA, MUUGUZI, MUHIMBILI

UFAFANUZI KIFO CHA EVODIA KAPINGA MUUGUZI, MUHIMBILI. Kuna taarifa inasambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Marehemu Evodia Kapinga amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Corona na kwamba alikua akihudumia wagonjwa wa Corona. Marehemu Kapinga hajawahi kuhudumia wagonjwa wa wanaougua ugonjwa wa Corona Marehemu alikua akitoa huduma kliniki ya watoto wenye tatizo la afya ya akili iliyopo jengo la watoto. Marehemu ni mgonjwa wa siku nyingi aliyekua akisumbuliwa na MARADHI AMBAYO HATUWEZI KUYATAJA KULINGANA NA MAADILI YA TIBA. Jana jumamosi tarehe 18 Aprili, 2020 saa NNE USIKU marehemu akiwa nyumbani kwake Kimara, alizidiwa ambapo watoto wake walifanya jitihada ya kumkimbiza Muhimbili lakini wakiwa njiani hali yake ilibadilika ndipo walipompeleka Hospitali ya karibu ya Sinza, Palestina. Madaktari na Wauguzi walifanya kila jitihada kuokoa maisha yake bila mafanikio ambapo amefariki leo jumapili saa 09 alfajiri. Hivyo, taarifa zinazosambaa kuwa kifo chake kinatokana na ugonjwa wa Corona siy...