Willian kwenda Man United Imefahamika kuwa tayari mazungumzo yameanza kati ya wawakilishi wa Man United na Willian kutoka Chelsea. Willian amekuwa katika kiwango bora sana katika miaka yake yote 5 akiwa na the blues lakini ikaanza kujitokeza tofauti kati yake na meneja wake Antonio Conte. Hali ilionekana kuwa mbaya zaidi pale Conte alipomwacha kwenye kikosi cha Chelsea kilichopambana na Man United kwenye fainali ya FA Cup. Meneja wa Man United yuko tayari kuhakikisha anapata saini ya Willian na kumuunganisha kwenye kikosi chake cha msimu wa 2018-2019.
Brings You Global News!