Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2018

Arsene Wenger Akabidhiwa zawadi ya End of Season Silverware na Sir Alex Ferguson kwa niaba ya MUFC

Arsene Wenger amekabidhiwa zawadi na Sir Alex Ferguson ya end of season silverware pale Old Trafford. Kabla mechi haijaanza Arsenal vs Man United, trip ya mwisho ya Wenger ya Old Trafford akiwa meneja wa Arsenal, Ferguson alimkaribisha na kumkumbatia, akimkabidhi zawadi kwa niaba ya Man United wakimshukuru na kumpongeza kwa miaka yake 22 katika football ya Uingereza. Hayo yalishuhudiwa na meneja wa sasa wa United José Mourinho akiiwakilisha United.

MAN UNITED 2-1 ARSENAL. WENGER APIGIWA MAKOFI YA BYEBYE NA MASHABIKI WA UNITED. FERGUSON AMKABIDHI ZAWADI WENGER HUKU MOURINHO AKIWA MTULIVU AKISHUHUDIA.

Manchester United 2-1 Arsenal Marouane Fellaini anafungwa kwa kichwa dakika za majeruhi 90+1 na kuwapatia United goli la pili na la ushindi baada ya Henrikh Mkhitaryan kusawazisha goli la Paul Pogba. -Konstantinos Mavropanos anacheza kwa mara ya kwanza mechi yake ya premier league akiwa Arsenal. -Paul Pogba anafunga goli la kwqnza katika kipindi cha kwanza baada ya Alexis Sanchez kupiga kichwa na mpira kugonga mwamba na kurudi. -Romelu Lukaku alilazimika kutoka baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Marcus Rashford mapema kipindi cha kwanza. -Dakika 6 baadae kipindi cha pili Mkhitaryan anasawazisha goli dhidi ya timu yake ya zamani. -Rashford anafunga goli lakini linakataliwa kwa kuwa ni offside. -Na hatimaye Sub Marouane Fellaini anavunja upinzani wa vijana wa Wenga na kuipatia ushindi United kwa kufunga kwa kichwa goli la pili.

FELLAINI AKATAA KUBAKI UNITED. AKATAA DAU LA PAUNI 140,000

Kiungo wa Manchester United ameonesha dhahiri kuwa yupo tayari kuondoka Old Trafford akiwa amemaliza mkataba wake. Imeripotiwa kuwa mwezi uliopita alishakutana mara tatu na bosi wake José Mourinho na akapewa dau la mshahara wa pauni 140,000 lakini aligoma. Mshahara wake kwa sasa ni pauni 80,000 kwa wiki. Fellaini amesema kuwa wakati wake wa kuwa Old Trafford umefika kikomo na sasa ni bora aondoke. Club kadhaa ulaya zinamuwania Fellaini zikiwemo, Juventus, PSG, West Ham, Leicester City, nk na ameona ni bora aondoke kwani pamoja na kubadilisha mazingira lakini atapata faida ya kuweka kibindoni mshaharakwa wiki mara mbili ya anaopata sasa.

Paul Pogba Awaomba wenzake kupambana kesho dhidi ya Arsenal

Paul Pogba Awaomba wenzake kupambana kesho dhidi ya Arsenal Akiongea katika mahojiano na Skysports, kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amesema na kuwataka wenzake kupambana vilivyo dhidi ya Arsenal watakaopambana nao kesho Jumapili dimbani Old Trafford katika mchezo wa premier league. Katika mechi ya awali mzunguko wa kwanza, Arsenal walifungwa nyumbani kwao kwa 3-1 huku Pogba akitoa assist 2 na badae akitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya. Pia Pogba ameshangazwa na kitendo cha baadhi ya wadau wa soka kuwasifia viungo wengine kwenye soka la Uingereza na kumponda yeye. United wamekuwa wazuri msimu huu na hadi sasa wanashikilia nafasi ya pili nyuma ya Mahasimu wao wa jadi Manchester City ambao tayari wameshatangazwa mabingwa baada ya kufikisha point ambazo hazitafikiwa na timu yoyote. Hivi karibuni wamecheza na Chelsea, Man City na Spurs na kuzifunga zote huku wakitokea nyuma na kushinda mechi. Kesho ndio kesho pale Mourinho atakapomkaribisha na kumwaga Wenger. Je uha...

Premier League today. Crystal Palace wawaadabisha Leicester City huku Liverpool wakishindwa kutamba mbele ya Stoke City, picha na matokeo mengine

Mechi kadhaa za Premier League zimepigwa jioni ya leo na haya ndio matokeo ya mechi hizo. Swansea City 0 Chelsea 1 Liverpool 0 Stoke City 0 Crystal Palace  5 Leicester City 0 Burnley 0 Brighton 0 Newcastle 0 West Brom 0 1 Huddersfield 0 Everton 2 Southampton 2 Bournemouth 1

José Mourinho Kumuaga Arsene Wenger Jumapili hii. Je, nini kitatokea? Uhasama utaendelea?

Kwa mara nyingine tena Manchester United na Arsenal zitakutana Jumapili hii kwenye awamu ya pili ya mchezo wa premier league. Mchezo huo utakaopigwa kwenye dimba la Old Trafford unatarajiwa kuwa mkali na mzuri kama ilivyokawaida zikutanapo timu hizi mbili. Hasa ikizingatiwa uhasama na upinzani wa hali ya juu uliopo kati ya meneja wa Arsenal, Wenger, na meneja wa Manchester United, Mourinho. Akihojiwa na vyombo vya habari, Wenger amesema anataka kuondoka kwa amani kwa hivyo anatarajia makaribisho mazuri toka kwa Mourinho na mashabiki wa soka wa Man United pale Old Trafford. Lakini pia aliongeza kuwa kuondoka kwake Arsenal hakuna maana kuwa timu hizi na makocha hawa hawatakutana tena kwani tayari amepata maombi toka timu mbalimbali zikimtaka kukochi kwa hiyo yeye anaondoka Arsenal lakini hastaafu. Pia aliongeza kuwa kwa kifaransa neno goodbye wao husema, 'au revoir' akimaanisha tutaonana tena. Wenger na Mourinho wamekuwa wapinzani wakubwa kwenye kazi ya ukocha tangu Mourinho a...

Manchester United Wamsajili Martin Svidersky Kutoka Slovakia

Mambo ya usajili yameanza kupamba moto baada ya club ya Manchester United kukamilisha usajili wa kiungo kinda kutoka Slovakia Martin Svidersky. Svidersky mwenye umri wa miaka 15 amesaini mkataba wa miaka mitatu hadi 2021 na atajiunga na kikosi cha Manchester United cha under 18 kuanzia msimu ujao. United wamewazidi kete Chelsea, Liverpool, Celtic, Man City, Inter Milan na Borussia Dortmund ambao walikuwa pia wakimwania mchezaji huyo. Martin Svidersky anaongea lugha tano ambazo ni Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa, Kigiriki, na Kislovakia ambayo ndo lugha ya kwao.

#BREAKINGNEWS: BASI LA POLISI LAGONGANA NA NOAH LIKITOKEA DODOMA! ASKARI 6 WAJERUHIWA VIBAYA NA WAWILI WA KWENYE NOAH WAFARIKI PAPO HAPO

Bari la polisi lililokuwa likitokea Dodoma lililobeba askari waliokuwa kwenye parade limepata ajali Morogoro Mikese Maseyu baada ya kugongana na Noah. Inasemekana askari sita wamejeruhiwa vibaya na watu wawili waliokuwa ndani ya noah wamekufa papo hapo. Mungu awalaze mahali pema peponi. Amina!

Arsenal na Atletico Madrid Watoshana Nguvu Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Europa League: Lacazette 1, Griezmann 1.

Hajatokea mbabe katika mchezo wa Arsenal dhidi ya Atletico Madrid uliopigwa jana usiku. Mchezo huo ulikuwa ni wa kwanza katika michezo miwili ya nusu fainali ya Europa League. Alikuwa ni Lacazette aliyowapatia Arsenal matumaini baada ya kupachika bao kunako dakika ya 61 na kuamsha shamrashamra kwa mashabiki wa Arsenal waliofurika uwanjani kushuhudia timu yao na kuona kama itawapatia matumaini ya kutinga fainali na hata kutwaa ubingwa wa Europa. Lakini matumaini ya Arsenal yakaingia mashakani mara baada ya Griezmann kusawazisha bao kunako dakika ya 82. Atletico hao pia walipata pigo mapema sana baada ya mchezaji wao mmoja kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye dakika ya 10 na kuwafanya kucheza wakiwa 10 uwanjani kwa takribani dakika 80. Picha zaidi za mechi

UCL first leg semi final: Bayern Munich 1-2 Real Madrid

Magoli yaliyofungwa na Marcelo pamoja na Assensio katika mchezo uliochezwa usiku wa Jumatano wa nusu fainali ya UCL  tayari yametoa faida kwa Real Madrid. Wanapata advantage ya magoli mawili ya ugenini na kuwafanya waichungulie fainali ya UCL.