Kiungo wa Manchester United Paul Labile Pogba amemsihi meneja wake Jose Mourinho asimpumzishe kwa sababu ya kuhifia kwamba bado hayuko fit kimchezo ama kuhofia kwamba atamchosha. Pogba ambaye ametoka kupata nafuu ama kupona kutokana na majeraha aliyoyapata zaidi ya miezi miwili aliliambia gazeti la Manchester Evening News kuwa kuelekea mechi na Arsenal ni lazima apate nafasi ya kucheza muda wa kutosha kwani amekuwa mwanasoka kwa sababu hiyo na pia anafurahia kucheza. Mourinho hatakuwa na budi kumchezesha Pogba muda wa kutosha ukizingatia kutokuwa fit kwa Nemanja Matic na Fellaini. Na Pogba ambaye ameahacheza dakika 90 katika mechi 2 amekuwa mhimili mkubwa kwenye kikosi cha United katika eneo lake la kiungo! Akuleta ari kubwa ya mchezo kwa wenzake. Kikosi cha Manchester United kitasafiri kwenye Emirates kukwaana na Arsenal siku ya Jumamosi katika kampeni za kuwania ubingwa wa Ligi ya Uingereza. Kikosi hicho kilicho chini ya Jose Mourinho kipo Katika nafasi ya pili nyuma ya Manch...
Brings You Global News!