Skip to main content

Posts

Showing posts from March, 2018

PAUL POGBA NA OUSMANE DEMBELE WABAGULIWA ST PETERSBURG RUSSIA

PAUL POGBA NA OUSMANE DEMBELE WAKUTANA NA UBAGUZI WA RANGI HUKO ST PETERSBURG RUSSIA FIFA bado wanafanya uchunguzi kuhusu tuhuma zinazowakabili mashabiki wa soka wa Urusi baada ya kudaiwa kuwaita Paul Pogba na Ousmane dembele nyani wakati wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Ufaransa dhidi ya Urusi ulioisha kwa Urusi kuchapwa magoli 3-1. FIFA bado wanaendelea kukusanya taarifa kutoka kwa wasimamizi mbalimbali wa mchezo huo kabla hawajatoa maamuzi. #AbelRkayUpdatea

CR7 AWATAKA REAL MADRID WAMSAJILI MO SALAH NA SIO EDEN HAZARD

CR7 AWATAKA REAL MADRID WAMSAJILI MO SALAH NA SIO HAZARD Inasemekana Cristiano Ronaldo anavutiwa Sana na mshambuliaji wa Liverpool na kwamba anataka uongozi wa Real Madrid waache mpango wao wa kutaka kumsajili Eden Hazard wa Chelsea na badala yake wamsajili Mohamed Salah kama sio kipindi hiki cha majira ya joto basi msimu ujao. Eden Hazard amekuwa akikosolewa mara kadhaa juu ya ubora wake kwani hajakaa katika huo ubora kwa muda wa kutosha kuweza kishawishi mashabiki wa soka. Pia wengi wanasubiri ujio wa kombe la dunia ili waone ubora wake haswa pale atakapoipigania nchi yake ya Ubelgiji ili basi aweze kufunga vinywa vya wanaomkosoa kuhusu kiwango chake. #AbelRKayUpDates

FT: TAIFA STARS 2 DRC 0. #SAMATTA NA #KICHUYA

FT:  TAIFA STARS 2, DRC THE LEOPOLDS 0 TAIFA stars leo wamewatoa watanzania kimasomaso baada ya kuwaadabisha The LEOPOLDS DRC kwa kuwaburuza kwa magoli 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa kwenye dimba la Taifa jioni leo. Hadi kipindi cha kwanza kinaisha hakukuwa na timu yoyote iliyoona lango la mwenzake. Lakini kunako kipindi cha pili timu zote mbili zikicheza mpira wa umakini zaidi huku zikiviziana na kushambuliana kwa zamu ilishuhudiwa Mbwana Samatta akiandika bao la kwanza kwa Stars na huku dakika zikiyoyoma Shiza Kichuya akaipatia Stars goli la pili. Naweza kusema leo Stars wamecheza mpira wa kujituma na kujiamini na wenye akili na usikivu toka kwa kocha wao huku Yondani, Nyoni na Gadiel wakiongoza safu ya ulinzi yenye umakini sana; na Samatta,  Kichuya na Simon Msuva wakiisumbua vibaya sana lango la wakongoman. Kabla mechi ya leo,  Stars walipambana na Algeria na kuambulia kipigo cha 4-1 wakiwa ugenini. #Hongera #TaifaStars

NEYMAR JR AMFAHAMISHA MESSI KWANZA KUHUSU KUHAMIA REAL MADRID

NEYMAR JR AMFAHAMISHA MESSI KWANZA KUHUSU KUHAMIA REAL MADRID Baada ya kutoka Barcelona na kuhamia PSG,  imejulikana kuwa Neymar JR hajawa mwenye furaha na yuko na mikakati ya kuhama mwisho wa msimu ili aende Real Madrid. Inasemekana kuwa lengo lake hilo ameamua kumjulisha Lionel Messi kwanza kabla haijawekwa wazi.

LIONEL MESSI AWATAKA BARCELONA WAMSAJILI MARCOS ALONSO WA CHELSEA

LIONEL MESSI AWATAKA BARCELONA WAMSAJILI MARCOS ALONSO WA CHELSEA FC Baada ya mechi ya Barcelona vs Chelsea kwenye 2nd leg mechi ambayo FC Barcelona waliwatwanga the Blues 3-0,  Lionel Messi ameibuka na kudai kuwa alivutiwa sana na ukabaji wa beki wa Chelsea Marcos Alonso ingawaje aliwanyanyasa na kupachika magoli mawili peke yake. Sasa baada ya kuvutiwa na beki huyu ameamua kuchukua hatua na kuwaomba wakubwa wake kumsajili Alonso ili kuimarisha eneo la ulinzi kwa timu yake huku ikijulikana kwamba Messi anatarajiwa kuukwaa ukepteni pale Andrés Iniesta atakapostaafu. Marcos Alonso amejizolea sifa na umaarufu wa kutosha kwani amekuwa beki imara asietikiswa ovyo ovyo. Pia amekuwa mpiga free kick mzuri sana mwenye kupachika magoli ya mtindo huo. Huyu beki Marcos Alonso hata ningekuwa mimi ni kocha ningemsajili.

Alaa Kumbe!!! WACHEZAJI WA CHELSEA WALICHUKIA KITENDO CHA KOCHA WAO KUMFWATA NA KUMKUMBATIA LIONEL MESSI

Alaa!!!  Kumbe!!! WACHEZAJI WA CHELSEA WALICHUKIA KITENDO CHA KOCHA WAO KUMFWATA NA KUMKUMBATIA LIONEL MESSI. Habari zimevuja kuwa ile siku ambayo Chelsea walifurumushwa kwa aibu nje ya mashindano ya champions League kwenye hatua ya 16 bora, kocha wa Chelsea, Antonio Conte aliwaudhi vibaya sana wachezaji wake. Kivipi? Baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa, Antonio Conte alienda na kumfwata Lionel Messi na kumpongeza kwa soka lake matata na mahiri na kisha kumkumbatia. Kama hiyo haikutosha, Conte alirudi tena mara ya pili na kuzungumza na Messi. Dah basi kitendo hichi kiliwaudhi saaana wachezaji wake. Conte mwenyewe alisema kuwa ni vizuri na inapendeza kumpa pongeza kwani alistahili kwa soka aliloonesha. Kwa kukukumbusha tu, Lionel Messi alifunga mabao mawili siku hiyo huku yote yakipita katikati ya miguu ya Thibaut Courtois aka doba na huku akitoa msaada (assist)  kwa goli la Ousmane Dembele. Haya bhana hayo ni ya Chelsea Football Club.

Alvaro Morata nje ya kikosi cha Spain

Alvaro Morata atupwa nje ya kikosi cha Spain Katika maandalizi ya mashindano ya kombe la dunia kocha Spain ameamua kumuacha nje ya kikosi Alvaro Morata kutokana nakutokuwa kwenye fomu nzuri huku ikijulikana kuwa mara ya mwisho tangu afunge goli ilikuwa boxing Day mwaka jana. Pia mchezaji huyo amesumbuliwa na majeraha mara kadhaa. Wakati huo anapata wakati mgumu kudumu kwenye kikosi cha kwanza tangu ujio wa Olivier Giroud. Spain wanatarajiwa kupambana na Ujerumani na Argentina kwenye mechi za kirafiki kujiandaa na fainali za kombe la dunia zitakazofanyika Urusi kuanzia Juni 14 mwaka huu

Jurgen Klopp anena baada ya kupangwa Robo fainali ya UCL na Manchester City

BAADA YA LIVERPOOL KUPANGWA NA MANCHESTER CITY KWENYE ROBO FAINALI YA UCL, JE, KLOPP AMESEMAJE? Jurgen Klopp,  kocha wa Liverpool amefunguka kuhusiana na timu yake kupangwa kupambana na Manchester City kwenye robo fainali ya UCL. Amesema,  "Nilishasema awali na bado ni ukweli, siku zote ni Hawaiian kwenye droo kwamba utapangiwa jirani yako, lakini kusema ukweli mimi wala sijali kabisa,  nikama ilivyokuwa awali tu. Tutapambana na tuliyepangiwa ambaye ni Manchester city. Twende kazi. Tumepoteza mara moja na kushinda mara moja dhidi yao kwenye ligi. Na sidhani kama kabla ya droo wangepangiwa Liverpool. Labda sisi sio timu nzuri kwenye 8 Bora lakini katika 8 Bora hakunaga mbabe labda timu mbili tu Barcelona na Bayern Munich lakini asente Mungu huu ni mpira na hakuna matokeo kabla ya mechi. Tuna mechi chache za kucheza hadi huo muda ufike lakini tunasubiria na tutajitoa kwa nguvu zote. Haya hayo ni ya Klopp tusubiri kwa Guardiola atasemaje.

Marouane Fellaini: I am not an aggressive player

Marouane Fellaini:  Mimi sio mchezaji mkorofi wa mtukutu.  I'm not an aggressive player,  says Marouane Fellaini. Kiungo wa Manchester United Marouane Fellaini amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye sio mchezaji mkorofi wala mtukutu awapo uwanjani. Amedai kuwa kazi yake yeye awapo uwanjani ni kuhakikisha kuwa anaunasa mpira uliopotea na kuurudisha kwenye imaya yao na ndio maana huwa anapata maonyo ya yellow kadi mara kadhaa. Amesema kuwa wengi hudhani kuwa yeye ni muhuni kutokana na style ya uchezaji wake jambo ambalo sivyo.

Mourinho happy for Klopp not to be sent off

Mourinho happy for the referee not to send off Klopp. Mourinho Aridhishwa na kitendo cha refa kutompa adhabu Klopp kwa kutoka nje ya eneo lake. Katika mchezo uliopigwa Jumamosi Manchester United vs Liverpool FC, kocha Jurgen Klopp alikasirishwa na ukabaji wa beki wake Lovren na hivyo kuanza kufoka kwa hasira na kujikuta ametoka nje ya eneo lake.  Kitendo hicho kilisababisha refa amwendee na kuzungumza nae ili kumtuliza lakini hakumpa adhabu ya kutoka kwenye bench. Kocha wa Manchester United akihojiwa na vyombo vya habari alisema kuwa japo wasingeamini lakini yeye alifurahishwa na refa kutomtoa Klopp kwenye benchi.  Mou aliongeza kusema kuwa jambo kama hilo lilimtokea yeye kwenye mechi kati ya crystal Palace na Manchester United pale beki wake alipofanya ndivyo sivyo alimfokea na bila kujua akajikuta ametoka nje ya eneo lake lakini refa hakumpa adhabu zaidi ya kuzungumza nae tu juu ya kosa hilo.

Arsenal wamimina risasi kwa Watford

Arsenal wawamiminia Watford FC risasi za kutosha Katika mchezo wa premier League uliochezwa leo jioni Arsenal wamewabugiza Watford bila huruma kwa kuwachabanga magoli 3-0. Magoli yao yalifungwa na Mustafi,  Aubameyang na Mkhitaryan. Ushindi huu ni kama kisasi kwao kwani kwenye mzunguko wa kwanza Watford walinyanyasa Arsenal na kuondoka na point zote. Ushindi huu pia umekuja baada tu ya kushinda mchezo wao dhidi ya AC Milan kwenye mashindano ya UEFA Europa League lakini kabla ya hapo walishapoteza mechi 3 mfululizo zikiwemo 2 za premier League na moja ikiwa ni fainali ya Carabao Cup dhidi ya Manchester City.

Manchester United fans loved the way Eric Bailly skinned, pocketed and embarrassed Mohamed Salah. Check out what their tweets.

FT: CHELSEA 2 CRYSTAL PALACE 1

FT:  CHELSEA 2 CRYSTAL PALACE 1 Chelsea walipambana jana na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 2 yaliyofungwa na Mbrazili Willian na huku lingine likitolewa zawadi baada ya Palace kujifunga huku Patrick akitupia moja kwa timu yake. Katika mzunguko wa kwanza the Blues walilala mbele ya palace na hivyo kuwafanya Chelsea kulipa kisasi jana. Katika mchezo huo Cesc Fabregas alitangazwa kuwa man of the match. Chelsea sasa wamepunguza pengo la pointi kati yao na Tottenham Hotspur nakuwa 2 pekee huku wakisalia nafasi yao hiyo hiyo ya 5.

MANCHESTER UNITED 2 LIVERPOOL 1. HATIMAYE JOGOO MWEKUNDU AGEUKA MTETEA MBELE YA SHETANI MWEKUNDU. FINALLY, THE RED COCK TURNS INTO A HEN BEFORE THE RED DEVIL 😈 2 goals by Rashford were enough to make the gap of 5 points between the two.

MAN UNITED vs LIVERPOOL FC #EPL E. AFRICA TIME 1530. NANI KULIA NA NANI KUCHEKA LEO. ASITOROKE MTU. TUKUTANE MIDA.

MANCHESTER UNITED WAANZA KUMNYATIA SAMWEL UMTITI WA BARCELONA

MANCHESTER UNITED WAANZA KUMNYATIA SAMWEL UMTITI Beki mstaarabu na mtulivu awapo uwanjani wa Barcelona Samwel Umtiti ameanza kudai nyongeza ya mshahara na kutaka mara mbili ya anacholipwa sasa lakini uongozi wa Barcelona umeonekana kulegalega kwenye maamuzi na kutoa mwanya kwa club ya premier League ya Manchester United kuanza kufanya mazungumzo na mwanasoka huyo juu ya kumsajili mnamo kipindi cha majira ya joto.