Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2018

CR7 UEFA FORWARD OF THE SEASON

CR7 UEFA Forward of the Season Kwenye droo ya leo Alhamisi ya champions league group stage, Cristiano Ronaldo ametunukiwa kuwa mshambuliaji bora wa msimu uliopita wa UEFA.  Ronaldo alikuwa mfungaji bora kwenye mashindano hayo akiwa na magoli 15 huku akiwa mshambuliaji tegemezi wa club yake ya Madrid msimu uliopita.  Magoli yake yaliisaidia Real Madrid kushinda taji la club bingwa ulaya kwa Mara ya tatu mfululizo na la nne ndani ya miaka mitano, huku likiwa ni la tano kwa Ronaldo.  Moja ya goli lake Kali sana alilofunga dhidi ya Juventus likiitwa bicycle kick likitajwa kuwa goli bora la msimu akimshinda mwenzake Gareth Bale aliyefunga la kufanana nalo.  Lionel Messi hakutajwa kabisa kugombea tuzo hii badala yake alikuwa ni Mohamed Salah aliyepata nafasi ya pili huku akiachwa mbali sana na Ronaldo pamoja na kuibeba Liverpool hadi fainali za champions league.   Ronaldo sasa ameachana na Madrid na amejiunga na Juventus huku akiwa na matumaini ya kuwndeleza ushindi.

"JOSÉ MOURINHO NI BORA APIGE KIMYA TU"-SVEN-GORAN ERIKSSON

"José Mourinho ni bora apige kimya tu." - Sven-Goran Eriksson Aliyewahi kuwa meneja wa kikosi cha taifa cha England Sven-Goran Eriksson anaamini kuwa meneja wa Manchester United, José Mourinho anakosea pale anapojibu shutuma au hukumu toka vyombo vya habari, na kwamba ingefaa abakie kimya.  Msweden huyo siyo mgeni kwenye hukumu, shutuma za vyombo vya habari vya England kwa sababu aliwahi kukutana na adha kama hizo wakati alipokuwa kocha wa England kwa takribani miaka minne.  José Mourinho amekutyana na adha kama hizo katika miaka yake ya ukocha kwenye premier league na inaonekana kwamba mambo yamekuwa mabaya zaidi baada ya Mourinho kuondoka kwenye kikao na wanahabari baada ya timu yake Man United kubugizwa bila huruma wala aibu kwa 3-0 wakiwa nyumbani Old Trafford mechi iliyopigwa usiku wa jumatatu iliyopita.  "Siku zote mambo yako hivyo, unapokosolewa kama kocha ni bora ukae kimya" alisema Sven-Goran Eriksson akiliambia 'Sky Sport'  "Usijaribu kujitete...

PEREIRA YUKO TAYARI KUPAMBANIA NAMBA UNITED-MOURINHO

Mourinho Anaamini Kuwa Pereira Sasa Yupo Tayari Kupambania Namba at Old Trafford Mourinho amefunguka na kusema kuwa kwa sasa Pereira wamepata nguvu ya kiakili kwa ajili ya kupambania position kwenye kikosi cha Man United.  Kiungo huyo wa miaka 22 ameshacheza kwenye mechi zote mbili za premier league za United na tayari ameitwa kwenye kikosi cha Brazil kwa Mara ya kwanza kwa ajili ya mashindano ya UEFA Nations League dhidi ya USA na El Salvador.  Boss huyo wa United ameweka wazi kuwa kwa Pereira kucheza misimu miwili nchini Hispania akiwa Granada na Valencia kwa mkopo kumemsaidia sana kujijenga kiakili kisoka.  "Sikufurahia kwa kutokucheza kwenye namba yake alipokuwa Valencia", Mourinho alisema.  " Lakini na maono ya kibinadamu ilimsaidia sana kupata ujuzi, amekuwa mwanaume sasa na ana utayari kiakili na kimwili." "Halafu likaja swala la Premier league Kumchezesha nafasi ambao tunadhani inamfaa zaidi, kumwelimisha na kumfanya aielewe nafasi yake."  "Ku...

Liverpool Waambulia goli moja toka kwa Brighton

Mohamed Salah akiifungia Liverpool goli moja na la pekee kwenye mechi hiyo na kuwakwelesha hadi namba 1 kwenye msimamo wa ligi. 

Epl side: Hatimaye Arsenal wapata ushindi wa kwanza. Arsenal 3-1 West Ham

Epl side: Hatimaye Arsenal wapata ushindi wa kwanza. Arsenal 3-1 West Ham.  Hatimaye vijana wa Unai Emery wamepata ushindi wa kwanza kwenye Mechi ya Epl leo jioni baada ya mashuti toka kwa Nacho Monreal, Danny Welbeck na Issa Diop(la kujifunga) kuzama wavuni na kuleta ushindi kwa Arsenal kwenye London derby hiyo.  Lakini alikuwa ni Marko Arnautovic aliyewainua mashabiki wa West Ham baada ya kupiga shuti la chini lililomshinda Kipa Peter Cec na kuwafanya wageni hao wa Arsenal kupata goli pekee kwenye mechi hjiyo

Epl side: Hatimaye Simba Avutwa Mkia. Man City 1-1 Wolves

EPL SIDE: MAN CITY WAFANYA KUFURU. FT: MAN CITY 6, HUDDERSFIELD 1. AGUERO APIGA HAT TRICK

EPL SIDE: MAN CITY WAFANYA KUFURU. FT: MAN CITY 6, HUDDERSFIELD 1. AGUERO APIGA HAT-TRICK - Sergio Aguero akiuchop mpira alioupokea toka kwa Kipa wake Ederson na kuandika bao la kwanza.   - Dakika tano badae Man city wakapiga la 2 kupitia Gabriel Jesus na Aguero akapiga la tatu.  - Jon Stankovic akaipatia Huddersfield bao huku David Silva akiandika la tatu kwa man city kwa free kick maridadi sana.  - Aguero akaikamilisha hat trick kabla hajatolewa huku Leroy Sané akiimyanyasa ngome chovu ya Huddersfield na kuandika bao

EPL SIDE: MAN UNITED WALA KISAGO TOKA KWA BRIGHTON. FT: BRIGHTON 3, MAN UNITED 2

EPL SIDE: MAN UNITED WALA KISAGO TOKA KWA BRIGHTON. FT: BRIGHTON 3, MAN UNITED 2 Kikosi cha José Mourinho kimepokea kichapo kikali toka kwa Brighton katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa Epl uliopigwa leo jioni.  - Glenn Murray akifungua akaunti ya ambao  kwa Brighton & Hove Albion FC akimalizia kwa ustadi sana  na kumwacha De Gea asijue la kufanya.  - Seagulls akaongeza la pili  na kuwafanya United wazidi kuchanganyikiwa kama sio kujichanganya.  - Manchester United wakapata bao la kwanza  kupitia Romelu Lukaku kwa kichwa baada ya kazi nzuri ya Luke Shaw.  - Lakini muda mfupi kabla ya Half time Eric Bailly akagawa penati kwa wenyeji wao na ikafungwa na Pascal Gross na kufanya kuwa 3-1.  - Paul Pogba akaifungia United goli la pili kwa mkwaju wa penati baada ya Fellaini kuchezewa ndivyo sivyo eneo la Hatari.  Lakini haikusaidia chochote kwa United Kwani huo ndio ukawa mwisho wa mchezo.

SERIE A SIDE: CHIEVO 2, JUVENTUS 3

SERIE A SIDE: CHIEVO 2, JUVENTUS 3 GAME YA KWANZA KWA RONALDO IMEISHA KWA USHINDI KWA JUVENTUS.   - Juventus wame pata ushindi wao wa kwanza wa Serie A kwa urahisi wakiwa ugenini dhidi ya Chievo.   - Cristiano Ronaldo akipiga game yake ya kwanza huku akianza kama mshambuliaji wa mbele.   - Sami Khedira alifungua ukurasa wa magoli baada ya dakika tatu tu za !chezo kwa mpira uliotokana na free kick.  - Chievo wakapambana na hatimaye Mariusz Stepinski kufunga kwa kichwa. Wakarudi tena na kufunga kwa penati goli la pili na Emmanuele Giaccherini  - Leonardo Bonucci akaipatia Juve goli la kusawazisha na Federico Berardeschi akamalizia game kwa kuipatia Juve bao la tatu na la ushindi.  Wakati huohuo mashabiki nguli wa Juventus walisikika wakilalamika kwa nini Ronaldo hakufunga bao na wakaongeza kusema kuwa angekuwa amecheza dhidi yao angewafunga.

LA LIGA SIDE: BARCELONA 3, ALAVES 0. NI ZAMU YA PHILIPPE COUTINHO NA LIONEL MESSI

LA LIGA: BARCELONA 3, ALAVES 0. Ni Zamu ya Philippe Coutinho na Lionel Messi - Inaanza na Lionel Messi kugonga mwamba wa juu huku kipindi cha kwanza kikiyoyoma kwenye mchezo wa La Liga Jana Jumamosi jioni.   - Ndipo Barcelona wakamwingiza Philippe Coutinho aliyekiwa bench mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika tasa.  - Ndipo Lionel Messi akavunja ukimya  katika dakika ya 64 kwa kufunga goli kwa shuti la free kick under the wall.  - Coutinho naye akaja na kuongeza la pili dakika saba baadaye akiupachika mpira kwenye kona ya mbali kule anakotagia sio kuku tena bali kanga kama ilivyo kawaida yake. (Sijui kwa nini Liverpool walimuuza)  - Messi akarudi tena kwenye nyavu za Alaves na kufunga la pili na la tatu kwa Barcelona katika dakika ya lala salama kabisa na kupeleka ushindi mnono Nou Camp.

ARSENAL WAKUTANA NA KISAGO CHA CHELSEA. WALA 3-2

EPL: CHELSEA 3, ARSENAL 2 - Chelsea wamewapiga Arsenal kwenye London Derby leo usiku huku Marcos Alonso akifunga goli la ushindi.   - Pedro alikuwa wa kwanza kuzichungulia nyavu za Arsenal  baada ya dakika Tisa tu akipokea cross ya Alonso.  - Pierre-Emerick Aubameyang akikosa goli la wazi na rahisi la kusawazisha kabla ya Alvaro Morata kuongeza la pili kwa Chelsea.   - Henrikh Mkhitaryan akafunga goli la kwanza kwa Arasenal kuto!ea ndani ya box, huku Alex Iwobi akifunga la pili na KUWEKA mambo sawasawa yaani 2-2.  - Alonso akipata msaada mkubwa toka kwa Hazard akamaliza kazi kwa kuoiga goli la tatu na la ushindi kwa Chelsea na kuwafanya Arsenal wamalize mchezo wa pili wa Epl bila pointi.

UEFA SUPER CUP FINAL. FT: REAL MADRID 2- 4 ATLETICO MADRID

UEFA SUPER CUP FINAL. FT: REAL MADRID 2-4 ATLETICO MADRID  Saul Niguez and Koke extra time strikes clinch Super Cup for Europa League holders after thriller in Tallinn. - Striker Diego Costa opened the scoring for Atletico Madrid after just 49 seconds of the clash on Wednesday - Forward Karim Benzema eqgualised for Real Madrid on the half-hour mark following a cross by Gareth Bale -  Sergio Ramos put Real in front in the second half from the penalty spot after Juanfran handled the ball in area - Costa pulled the Europa league holders back into the contest in the 79th minute of the Uefa Super cup final   - Saul Niguez  put Atletico Madrid in first half of extra time with a stunning left-footed volley in the box  - Koke added a forth for Atletico Madrid in the 104th minute of the match to secure win over rivals

WILLIAN AFUNGUKA KUHUSU ANTONIO CONTE, AMESEMA.....

WILLIAN AFUNGUKA KUHUSU ANTONIO CONTE "Ningekuwepo Chelsea bado kama Conte Asingeondoka? La hasha" Afunguka Willian Kama Antonio conte angesalia kama meneja wa Chelsea,  mbrazil anayekipiga chelsea, Willian amefunguka na kusema kwamba yeye angeondoka Stamford Bridge.  Willian anasema kuwa asingeweza kubakia klabuni hapo kama Antonio Conte angebakia kuwa meneja.  Nafasi ya Conte ilichukuliwa na muitalian mwenzake Maurizio Sarri huku akiwa in charge ameshuhudia timu yake ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Huddersfield kwenye mechi yao ya ufunguzi ya EPL iliyopigwa Jumapili ya jana.

JOSÉ MOURINHO KUWEKA KIBINDONI PAUNI MILIONI 12 ENDAPO ATATIMULIWA NA MAN UNITED

JOSÉ MOURINHO KUWEKA KIBINDONI PAUNI MILIONI 12 ENDAPO ATATIMULIWA NA MAN UNITED Meneja wa Manchester United José Mourinho ametajwa kama ataweza kuwa meneja wa kwanza kufukuzwa kazi kwenye Epl msimu huu, lakini Mreno huyo  anaweza asilalamike  endapo tukio hilo litatokea kwa kuwa package atakayoambulia si ya mchezo.  Kwa mujibu wa "The Sun", Mourinho anaweza kulipwa kiasi cha pauni milioni 12 kama atatemwa na United.

WILLIAN AGUSIA MUUNGANO WAKE NA MOURINHO

Willian Agusia muungano wake na Mourinho   José Mourinho na willian wameshashinda premier league wakiwa Chelsea, huku mbrazil huyo akiwa yuko tayari kufanya kazi kwa Mara nyingine na bosi wake huyo wa zamani.  Winga wa Chelsea, Willian amegusia kuwa angekuwa tayari kusaini Manchester United kwa kusema kuwa anataka kufanya kazi tena na José Mourinho.  Willian na Mourinho wameshinda Epl Mara mbili wakiwa pamoja pale Stamford bridge and willian amekuwa akihusishwa  Kwenda old Trafford.  Mourinho anatamani sana kuimarisha safu yake ya ushambuliaji huku kukiwa kumebakia siku chache tu kwisha kwa dirisha la usajili hapo Alhamisi 9 Agosti.  Willian pia amesema kuwa angefurahia kubakia Chelsea kwa msimu wa 2018-2019 lakini pia ameacha mlango wazi endapo uwezekano wa kuungana na Mourinho utakuwepo.  "Mourinho ni meneja mzuri ambaye haijawahi kutokea Mimi kufanya nae kazi. Tuna mahusiano mazuri nasi ni marafiki." Willian aliliambia ESPN Mbrazil baada ya Chelsea ...

COMMUNITY SHIELD: MAN CITY 2, CHELSEA 0. GAME ILIKUWA UROJO UROJO KWA MAN CITY

COMMUNITY SHIELD: MAN CITY 2, CHELSEA 0 Mabingwa watetezi wa Epl, Manchester city jioni ya leo wamewaadabisha vilivyo mithili ya kumchinja kuku mgonjwa asiyeweza hata kujitetea katika mpambano uliotarajiwa ungeleta ushindani wa hali ya juu lakini walaa.  Magoli ya man city yalifungwa na Sergio Aguero kunako dakika za 13, 58. Na hivyo man city kutwaa taji hilo la community shield ambalo ni kiashilio cha ufunguzi wa ligi ya Epl itakayoanza tarehe 10 Ijumaa ya wiki ijayo.

MAN UNITED BADO WANAWAZA DEAL LA KU SWAP MARTIAL NA WILLIAN

MAN UNITED BADO WANAWAZA DEAL LA KU SWAP MARTIAL NA WILLIAN  Kwa mujibu wa ripoti zilizotoka leo jumapili asubuhi, Manchester United wanaweza kujaribu kuwashawishi Chelsea kubadilishana wachezaji, Martial kwa Willian.  Willian amekuwa akiendelea kuhusishwa na kuihama Chelsea kipindi hili cha kiangazi, wakati mahusiano ya Martial na José Mourinho yakiwa sio mazuri kwa muda mrefu.  Kwa mujibu wa gazeti la Mirror kila timu imeweka gharama inayofanana ya mchezaji wake ikiwa ni kiasi cha pauni milioni 75, hii ikimaanisha kwamba ubadilishanaji wa wachezaji hawa unaweza kutokea.  Walakini, baada ya uhamisho wa Kwenda Barcelona kushindikana, willian amedai kuwa yeye bado anafurahia kubaki Chelsea. Na huku bosi mpya wa Chelsea Maurizio Sarri akiwa yuko tayari kufanya kazi na mbrazil huyo na anaweza kumpatia muda wa kucheza michezo mingi zaidi ikilinganishwa na alivyuofanya Antonio Conte.  Wachezaji hawa wawili wote waliwakorofisha mabosi wa baada ya willian kuchelewa kuj...