WAGONJWA 37 WAPONA CORONA, 71 WASUBIRI VIPIMO VYA MWISHO Wagonjwa 37 waliokuwa wameambukizwa virusi vya Corona #COVID19 wamepona na kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya vipimo vya mwisho kuthibitisha kwamba hawana maambukizi. “Watu hawa 108 hawana dalili zozote za ugonjwa kama vile homa au mwili kuchoka isipokuwa wapo katika vituo vya matibabu kusubiri vipimo vya mwisho ili kuthibika kwamba hawana virusi vya corona kabla ya kuruhusiwa kutoka vituoni,” amesema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. Waziri Ummy Mwalimu amewataka watu waliopona ugonjwa huo kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya ili kujikinga na maambukizi mapya ya COVID-19 kwani zipo tafiti zilizofanyika nchi mbalimbali ikiwamo China zimeonyesha kuwa watu wanaweza kupata maambukizi mapya kama asilimia 14. “Tunapenda kuwahimiza watu waliopona watoe elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) kwa jamii. Pia, Nitumie fursa hii kwa niaba ya Serikali kutoa shukrani ...
Brings You Global News!