Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2012

OLYMPIC MEDAL COUNT

Medal Count        Gold      Silver      Bronze China                       10         6              3 United States           7          7              5 Japan                        1          4              7 France                 ...

LILIVYOANDIKA GAZETI LA MWANANCHI KUHUSU "TUCTA" KUPINGA SHERIA YA PENSHENI

NIMELINUKUU GAZETI LA MWANANCHI " Limesheheni " SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) limeandaa maandamano ya amani kupinga mabadiliko ya  kupitishwa kwa sheria ya marekebisho ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA). Maandamano hayo yatafanyika Agosti 4 kuanzia viwanja vya Mnazi mmoja hadi katika Ofisi za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholus Mgaya alisema sheria ya mpya ya mifuko ya jamii inaeleza kuwa mfanyakazi mwanachama atakapotokea kuwa ameacha au ameachishwa kazi hawezi kuchukua mafao yake hadi atakapofikisha umri wa kustaafu ambao ni miaka 55 kwa hiari au miaka 60. Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholus Mgaya Alisema kuwa mfanyakazi mwanachama wa mfuko wowote wa hifadhi ya jamii, akiacha au akiachishwa kazi akiwa na miaka 35 inabidi asubiri kwa miaka 20 alipwe mafao yake ya uzeeni. “Hiki ndio kipelngele cha sheria ambacho kimeleta taharuk...

MBUYU TWITE KUZIBA PENGO LA YONDANI SIMBA!

Timu ya Simba wapo katika hatua za mwisho kumsainisha beki wa APR, Mbuyu Twite ili kuziba pengo la Kelvin Yondani aliyetimkia Yanga. Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi, Gedfrey Nyange Kaburu alisema:- "Ni mapema kutaja kiasi cha fedha tutakachotumia kukamilisha usajili wake, lakini wiki ijayo atatua nchi kwa lengo la kukamilisha usajili." alisema Kaburu. Twite mwenyewe alisema anashawishika kuja kusukuma kandanda lake Simba kwa sababu viongozi wa timu hiyo wamekwishazungumza naye. Gazeti la Mwananchi lilimnukuu mchezaji huyo akisema:- "Ukweli ni kwamba jana kabla hatujarudi nyumbani Rwanda nilikutana na watu wa Simba tukazungumza ili nije kuichezea timu yao, niliwaambia nipo tayari ingawa hatukufikia muafaka wa moja kwa moja.Hata hivyo, hakuna shaka kwamba mambo yatakwenda vizuri na hatutashindwana kwa vile binafsi napenda kuja kucheza Tanzania," alisema Twite. Lakini hakuwa tayari kutaja dau walilokubaliana na uongozi wa Simba. Liliandika gazeti la M...

BAHANUZ ATAMANI KUKIPIGA STARS

Yule mchezaji aliyesajiliwa na Yanga akitokea Mtibwa Sugar na ambaye aliibuka kuwa mfungaji bora wa michuano iliyomalizika hivi karibuni ya Kagame Cup, Said Bahanuz, amesema kuwa ni wakati muafaka kwake kukipiga taifa stars. Nikilinukuu gazeti la Mwananchi Bahanuz alisema, "Nafikiri kwa sasa tuna tatizo la ufungaji timu ya taifa, naamini nitakapopewa nafasi nitaendeleza haya niliyofanya Kagame na timu kupata ushindi."Aliongeza: "Siri yangu kubwa kuibuka mfungaji bora ni kwa sababu nilimtanguliza Mungu mbele kwa kila jambo na kujituma." "Nimezaliwa na kulelewa katika mazingira ya dini, ninamwamini zaidi mwenyezi Mungu kuliko chochote." "Sidhani kama kweli kuna uchawi kwenye soka, ni imani potofu za watu wachache, nimejipanga kufanya vizuri zaidi na siyo kuishia hapa." "Kila jambo nalofanya namtangulia Mungu, nafikiri ndiyo siri kubwa yangu kufanya vizuri kwenye mashindano ya Kagame." Alisema Source: Mwananchi

The Chinese Swimmer, Ye Shiwen Denies Using Drugs

China's 16-year-old swimming prodigy Ye Shiwen   has denied taking performance-enhancing drugs,  after smashing a world record at the London Olympics. She said her success was a result of hard work and training

MwanaHalisi Mwiko Mitaani

Serikali imelifungia gazeti la MwanaHalisi linalotoka kila wiki kwa kile ilichodai kutoa habari za uchochezi. Mkurugenzi wa mawasiliano katika wizara ya mawasiliano Fabian Rugaimukamu, akizungumza jana alisema kuwa kufungiwa huko kunaanza mara moja. Kwa mijibu wa Rugaimukamu, toleo la MwanaHalisi namba 302 la Julai 11-18, namba 303 la Julai18-24 na namba 304 la Julai  25-Agosti 01 mwaka huu na mengine yaliyopita yalichapicha habari za kuitisha jamii.  Bwana Saed Kubenea, Mhariri Mkuu wa MwanaHalisi Alisema pia kwamba muhariri wa gazeti hilo alishawahi kuitwa na kuonywa mara kadha lakini alikataa kutambua kwamba aliyoyaandika ndani ya gazeti lake hayakuendana na taaluma yenyewe. “Siku zote Muhariri alijilinda kwa kunukuu kifungu namba 18 cha katiba ya Tanzania kinachotoa uhuru wa kujieleza, lakini akaepuka kunukuu kifungu namba 30, kinachoonesha mipaka ya kujieleza." Alisema. Muhariri mkuu wa MwanaHalisi Saed Kubenea alisema alisikitishwa na serikali kwa kitend...

YANGA YAJIIMARISHA

Timu ya Yanga ambayo wiki iliyopita walichukua kwa mara nyingine kombe la Kagame baada ya kuichapa bila huruma timu ya Azam 2-0, imeendelea kujiimarisha kwa kumsainisha mchezaji maarufu Didier Kavumbagu kutoka Burundi. Gazeti la Championi liliandika kwamba baada ya kumtilisha saini msukuma kandanda huyo wa Burundi, imetangaza kufunga usajili na sasa kuelekeza nguvu zake kwenye maandalizi ya ligi msimu ujao. Mchezaji huyo anatarajia kurudi nchini keshokutwa ili ajiunge na wenzake kule Jangwani yalipo makao makuu ya wababe hao wa Afrika Mashariki na Kati. Kavumbagu ndiyo yule aliyeifungia Atletico ya Burundi magoli 2 ambayo yaliizamisha Yanga kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa kombe la Kagame. Nikilinukuu gazeti la Championi ambalo nalo lilimnukuu Seif Ahmed anayehusika na mambo ya usajili aliyesema:- “Kweli tumemalizana naye na ameishasaini kuichezea Yanga, yalikuwa ni maoni ya pamoja kati ya kocha na kamati yetu maalum. Kuanzia hapa nafikiri tutakuwa tumefunga usajili,” ...

ALIMANUSURA LULU ALE SUMU

Huyu ndiye Elizabeth Michael aka Lulu ambaye inasemekana  alimanusura apewe sumu baada ya jamaa mmoja kuonekana  gerezani Segerea akimpelekea chakula huku akijfanya ni ndugu wa karibu. Askari wa gerezani hapo walipomwona walimtilia shaka  na kuanza kumuhoji lakini alionekana kutokuwa na majibu sahihi  na kisha alitoweka. Gazeti la Ijumaa liliripoti siku ya tare 30 Julai 2012.     Hizi ni picha za Lulu akiwa kwenye mapozi mbalimbali katika life yake. Msanii huyo hadi sasa bado yupo segerea kwani kesi yake haiishi kuahirishwa  kutokana na sababu mbalimbali. Na pia hadi sasa bado umri wake unaleta utata kama ni mtoto,  yaani chini ya miaka 18, au mtu mzima, yaani miaka 18 na nane na zaidi.

MGOMO WA WALIMU HUO!!!

Walimu nchini Tanzania wameanza mgomo wao leo wakidai malipo mazuri wakiungana na madaktari kudai  nyongeza ya mishahara wakidai hali ya maisha kupanda. Shule nyingi za serikali zililazimika kusitisha ufundishaji kwa sababu walimu walibaki nyumbani. Walimu wapatao 200,000 nchi nzima walikubaliana kugoma huku wakipuuza onyo la Rais aliyedai mgomo huo siyo halali. Inasemekana yapata asilimia 95.7 ya walimu walipigia kura mgomo, hivyo kuufanya mgomo huo kuanza rasmi leo. Gratian Mukoba, Rais wa Umoja wa Walimu Tanzania Mr. Mukoba alisema kuwa hata kama serikali imewataka walimu kuripoti kazini na kufundisha, lakini hawatafundisha. Aliongeza kusema kuwa mgomo wao ni halali kwani walifuata taratibu zote ili ufanikiwe.

BRAZIL YAICHAKAZA BELARUS 3-1 OLIMPIKI

Mchezaji Neymar wa Brazil  jana alionesha ni kwa nini timu kubwa duniani zinamuwania kumsajili baada  ya Brazil kuwa nyuma kwa goli 1 na hatimaye kushinda 3-1 kwenye mchezo wa soka uliochezwa Old Traford Jumapili. Huku Neymar akiwa mchezaji muhimu sana kwenye mechi hiyo. Belarus waliishtua Brazil pale walipoanza kuongoza mchezo huo katika dakika ya 8 kwa goli  lililofungwa kwa kichwa na Renan Bardini Bressan  mbele ya umati wa watu wapao 66,000 kwenye uwanja wa wababe wa soka Manchester United. Lakini baadaye Brazil walipambana na kufanya mashambulizi ya nguvu yaliyoongozwa na Neymar ambaye katika dakika ya 65 alipiga mpira wa adhabu uliomshinda golikipa wa Belarus Aleksandr Gutor. Neymay akiwa anacheza katikati alimpatia krosi mchezaji wa AC Milan Pato aliyesawazisha. Brazil wakiwa wanaongoza, Neymar alimpatia pasi tena Oscar aliyefunga goli  la ushindi.   Mpambano mkali kati ya Brazil na Belarus Kabla ya mechi hiyo, ndani ya uwanja huo huo, M...

SPAIN YATOLEWA KWENYE SOKA OLIMPIKI

Timu ya soka ya Spain ambao ni mabingwa wa Ulaya na Dunia jana Jumapili ilitolewa nje ya mashindano kwenye Olimpiki ya 2012 baada ya kupigwa na timu ya Honduras 1-0  kwenye uwanja wa Newcastle"s St. James Park. Goli lililofungwa na Jerry Bengtson katika dakika  ya 7 ndilo lililowapeleka nje ya mashindano hayo wahispania hao waliokuwa kundi D. Bengtson aliruka na kufunga goli kwa kichwa baada ya kupokea krosi iliyochongwa na Roger Espionaza na kumpita golikipa anayesakata kabumbu Manchester United David de Gea. Picture source: AFP

MCHINA ALIYEVUNJA REKODI YA MITA 400 OLIMPIKI HUYU HAPA

  Anaitwa Ye Shiwen (16) kutoka China, alikimbia mbio za wanawake za mita 400  na kuweka rekodi ya dunia kwenye mashindano ya Olimpiki huko London, Uingereza siku ya Jumamosi. Alikimbia kwa dakika 4 na sekunde 28 na kuifuta rekodi ya awali ya dakika 4 na sekunde 29  iliyowekwa na Mu australia Stephanie Rice miaka minne iliyopita.

UGONJWA WA EBOLA WAUA 14 UGANDA

Ugonjwa wa ebola ambao unaua watu kwa haraka sana ulianza mwanzoni mwa mwezi Julai huko mashariki wa Uganda na tayari umeua watu 14. Shirika la afya duniani lilisema siku ya Jumamosi. Ugonjwa huo ulianzia mashariki mwa wilaya ya Kibaale, kama kilometa 200 kutoka mashariki mwa mji mkuu wa Uganda, Kampala, na kama kilimeta 50 toka mpakani na Nchi ya Kidemokrasia ya Kongo. "Tumethibitisha watu 20 kuambukizwa virusi vya ebola ambapo miongonimwao 14 wamekwishafariki" Alisema Joaqim Sewaka, mwakilishi wa shirika la afya duniani. Alisema pia kuwa timu za wizara ya afya Uganda na kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani, Centre for Disease Control (CDC), vimewasili eneo lililoathirika. Ugonjwa huo ulioitwa kwa jina la mto mmoja huko Kongo, uliua watu 37 mashariki mwa Uganda mwaka 2007 na watu 170 kaskazini mwa nchi hiyo mwaka 2000. Mgonjwa wa ebola akiwa anahudumiwa hospitalini

KABILA ACCUSES RWANDA FOR HELPING REBELS

Congo's President accused Rwanda of backing a new rebellion in Congo's east and called their support an "open secret”. President Joseph Kabila spoke to journalists late Saturday in a rare appearance and said that the government will investigate accusations that Uganda may also be backing the M23 rebellion in the east, though the country said it was not involved. <a href="http://adserver.adtech.de/adlink/3.0/1191/3111109/0/165/ADTECH;loc=300;key=key1+key2+key3+key4" target="_blank"><img src="http://adserver.adtech.de/adserv/3.0/1191/3111109/0/165/ADTECH;loc=300;key=key1+key2+key3+key4" border="0" width="250" height="250"></a> The uprising has brought the worst violence in years to the already volatile Congo. It has forced more than 260,000 people from their homes in the past three months. And it is draining the resource...

MIAKA 3 TANGU MICHAEL JACKSON AFARIKI. PICHA ZAKE 13 HIZI HAPA

Alijulikana kama mfalme wa pop duniani. Alikufa akiwa na miaka 50. Picha hizo zinaonesha matukio yake mbalimbali ya kimuziki  tangu akiwa mdogo hata mtu mzima.   Kifo chake kilishtua watu wengi sana  duniani na kuhuzunisha wengi pia.   Ni miaka mitatu sasa tangu afariki.  Lakini muziki wake mwanamuziki huyo aliyekwishawahi  kutembelea Tanzania miaka ya nyuma, bado unashika kasi duniani   Picha ya hapo juu ni siku ya mazishi yake,  watu wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi lake.   Picha hizi za utoto wake zikionesha kabla hajaamua  kujifanyia marekebisho ya sura  yake. Hii ni moja ya staili zake za kucheza ambazo  ziliwavutia watu wengi sana akiwa jukwaani Source: CNN

SNOOP DOGG MARUFUKU NORWAY

Mwanamuziki Snoop Dogg wa Marekani mwezi uliopita alizuiliwa kwenda nchini Norway kwa miaka miwili kutokana na kile kilichodaiwa kutaka kuingia nchini humo akiwa na Marijuana ama maarufu kama bangi. Dogg alitakiwa kufanya onesho huko Arendal, Norway tarehe 28 Julai wakati alipozuiliwa na maafisa wa mpakani baada ya mbwa wa kunusa madawa kumgundua. Alikutwa na gramu 8 za bangi kwenye begi lake pamoja na kiasi kikubwa cha fedha kinyume na taratibu. Baada ya kukubali kosa alitozwa faini ya dola 8,600. Mwanasheria wake alisema kuwa Dogg hana haja ya kukata rufaa yoyote. Snoop Dogg Mwanamuziki huyo raper ambaye anatarajia kutoa albamu ya rege mwishoni mwa mwaka huu itakayoitwa Snoop Lion , pia aliwahi kutiwa nguvuni huko Texas mwezi Januari wakati mbwa wa polisi walipomkuta na bangi kwenye begi chafuchafu ndani ya basi lake. Snoop Dogg

KOMPANY HATOKI MAN CITY!

Vincent Kompany amesaini mkataba wa miaka sita ndani ya timu yake ya Man City, mkataba  wa kwanza mrefu kusainiwa kwenye historia ya timu hiyo. Ni jambo lisilo la kawaida kwa timu hiyo kutoa ofa kwa wachezaji kusaini mkataba wa zaidi ya miaka mitano. Lakini mbelgiji huyo mwenye miaka 26 amekuwa mchezaji muhimu kwa Man City na alikuwa kepteni wa timu yake ilipotwaa ubingwa wa England msimu uliopita baada ya kuukosa kwa miaka 44. "Nimekuwa hapa tangu mwanzo na nimeona mabadiliko mengi ya timu na nayajua ya ndani na nje ya timu." Alisema Kompany ambaye alijiunga na timu hiyo mwaka 2008 kutoka Hamburg SV kwa donge la dola milioni 9.25. "Ni vizuri kujua kwamba nitaendelea kuwa Man City kwa miaka mingine sita.Najivunia kuwa timu yangu inanipenda." Aliongeza mchezaji huyo.   Vincent Kompany, mchezaji wa Man City

WANAFUNZI WAUA IRINGA

Wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi cha Bulongwa kilichoko Wilaya ya Makete mkoani Iringa, wamemuua kwa kumshambulia kichwani mkufunzi wa chuo hicho, Dk. Jumbe Mafingo, kwa madai ya kupinga jaribio lake la kutaka kumbaka mwanafunzi mwenzao. Taarifa za awali za makachero wa polisi zilieleza kuwa mkufunzi huyo aliuawa baada ya kutuhumiwa kwamba alitaka kumdhalilisha kijinsia mwanafunzi wa kike, Jean Laison Mwakabuta kwa kutaka kumbaka. Tukio hilo la kuuawa kinyama kwa mkufunzi huyo ambaye ni mwalimu wa nidhamu chuoni hapo, lilitokea juzi usiku nyumbani kwake mjini hapa. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, Dk. Mafingo alifikwa na umauti baada ya mwanafunzi huyo kuamua kwenda nyumbani kwake usiku ili kumkabidhi maelezo yake ya kimaandishi kuhusu sababu zilizomfanya alale nje ya chuo. Ilielezwa kuwa muda mfupi baada ya kuingia kwenye nyumba ya mwalimu huyo, mwanafunzi huyo alianza kupiga kelele kuwa anabakwa. Kamanda wa Polisi Mkoani Ir...

SPIKA AVUNJA KAMATI YA BUNGE

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda, jana aliivunja kamati ya bunge ya Niashati na Madini baada ya  kamati hiyo kutuhumiwa kuhusika na rushwa.   Spika Anne Makinda Wajumbe wa kamati hiyo wametuhumiwa na wabunge wenzao wiki hii kupokea rushwa toka kwa makampuni ya mafuta waliotaka wapewe tenda ya kusambaza mafuta kwa Independent Power Tanzania Limited (IPTL). Makinda lifikia hatua ya kuvunja kamati hiyo baada ya mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa kumwomba kufanya hivyo. Kwa mujibu wa Makinda, kamati zote zinazotuhumiwa kwa mwenendo mbaya zitafanyiwa uchunguzi na zikikutwa na mmomonyoko wa maadili zitavunjwa na kisha kuhojiwa na tume ya maadili ya bunge chini ya mwenyekiti wake Bregadia Jenerali Mstaafu Hassan Ngwilizi. Wajumbe wa kamati iliyovunjwa ni:- Seleman Zedi (mwenyekiti), Diana Chilolo (mwenyekiti msaidizi), John Mnyika (Ubungo -Chadema), Yusuf Khamis (Nungwi- CUF), Mariam Kisangi (viti maalumu- CCM), Catherine Magige (viti maalumu...

HAWA NDIYO YANGA, WABABE WA KAGAME CUP. EBU WACHEKI

  Picha ya kwanza na ya pili, ni kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kagame   Wachezaji wa Yanga wakiwa na furaha baada ya kutwaa Kombe la Kagame   Picha ya chini na juu, Yanga wakishangilia ushindi wa Kombe la Kagame.