Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2012

Berbatov Aenda Fulham

Hatimaye Dimitr Berbatov anahama Man United na kuelekea Fulham kwa donge la dola milioni 5. " Berbatov anamalizia vipimo vyake na kama mambo yataenda vema atakuwa moja ya wachezaji wetu. Kulikuwa na timu nyingi zilikuwa zinamuhitaji lakini sisi tulikuwa na uwezo wa kumpata. Alikuwa kwenye list yangu wakati wote. Nilijaribu kumfuatilia miezi kadhaa iliyopita lakini sikufanikiwa hivyo nilirudi tena na sasa ulikuwa ni wakati muafaka kwa yeye kufanya maamuzi." Alisema Martin Jol kupitia Fulham FC.com. Berbatov alienda Man United akitokea Tottenham Hotspur mwaka 2008 kwa rekodi ya uhamisho wa dola milioni 30, kitu ambacho kinaonekana hakijaendana na uwezo wake wa kazi awapo uwanjani. Lakini kama isingekuwa uwezo wake wa ajabu wa kipindi cha kwanza mwaka 2010-2011, Man United wasingeweka rekodi ya kuchukua kombe la ligi mara 19 msimu huo. Berbatov alikuwa kwenye msimu wa mwisho wa mkataba wake, na kwake yeye mwenye miaka 31 kupata mkataba wa dola milioni 5 siyo biasha

"Hatutamwongezea Mshahara Walcott," Asema Wenger

Arsene Wenger alisisitiza jana kwamba bado anajaribu kumshawishi Theo Walcott kusaini mkataba mwingine na Arsenal, lakini akamwambia winga huyo kwamba sheria za mishahara hazitapindishwa kwa sababu yake.   Theo Walcott Walcott ameruhusiwa kuendelea na mkataba wa mwaka mmoja wa mwisho, hatari ambayo Arsenal waliikwepa kipindi cha nyuma walipomuuza Robin Van Persie hivi karibuni na Samir Nasri mwaka jana. Walcott atakuwa huru kuondoka msimu ujao wa joto (summer) endapo mkataba wake utafika kikomo, lakini Wenger ana uhakika zaidi kwamba atabakia kuliko alivyowafikiria Van Persie na Nasri . " Theo ana miaka 23 tu, ni mwingereza, anaishi mwendo wa dakika 10 tu toka hapa. Hivyo natumaini tutafikia makubaliano." Alisema Wenger. Arsenal hawana mpango wa kulipa wachezaji viwango vya juu sana na Wenger aliweka wazi kabisa kwamba hivyo ndivyo ilivyo. "Kila maamuzi yana mpangilio wake na hicho ndiyo kiwango chetu cha mshahara na tunakiheshimu. Kama hatutafanya

Bangi Yakamatwa Namanga Ikitokea TZ..!!

Zaidi ya kilogramu 900 za bangi yenye thamani ya shilingi milioni 9 zilikamatwa jana Alhamisi na maofisa wa mamlaka ya mapato ya Kenya mpakani mwa Kenya na Tanzania. Haya ndiyo magunia ya bangi yaliyokuwa yanaingizwKenya  kutokea Tanzania Bangi hiyo iliyokuwa ndani ya magunia 31 ilikuwa ikisafirishwa kwa lori ambalo baada tu ya kukatiza mpaka kuingia Kenya maofisa walilitilia mashaka. " Maofisa walikuwa wakifanya ukaguzi wao wa kawaida tu wakati walipoikuta bangi imefichwa kwenye lori hilo ." Alisema msemaji wa Mamlaka ya Mapato Kenya bwana Kennedy Onyonyi. Dereva wa lori hilo alitoroka mara moja wakati polisi wakilikagua lori lake na wameamua  kufanya doria ya kumsaka maeneo ya Namanga , mpakani mwa Kenya na Tanzania. Kufuatia tukio hilo, polisi wa Kenya wamemua kuweka ulinzi mkali ili kuzuia uingizaji wa bangi nchini mwao kutokea Tanzania.

Baware/Chukua Tahadhari: OnLine Theft-Wizi Wa Kwenye Mtandao

Ukiziangalia e-mails hizi hapa unaweza kudhania utaibuka tajiri mkubwa Duniani. Kumbe ni janja ya baadhi ya majitu ambayo hayafanyi kazi bali kupanga mbinu mbalimbali za kuwaibia watu. Ona e-mails hizi hapa na Chukua Tahadhari. Dearest one, How are you today together with your business and your entire family?I guess that everything is OK with you. I know this mail will not come to you as a surprise since we have not had a previous correspondence,please bear with me. I am more than happy to read your interesting mail from site and i hope that you are fine and healthy, I have noticed that you are the kind of man i am looking for since all this while, i believe that you are a trust worthy and caring person, that's what makes me to disclose my identity to you.                   My  name is Miss Juliet Muse,23 years old   from Darfur Region of Sudan  and presently i am residing in the refugee camp here in Dakar  Senegal as a result of the  the killing of my family by the reb

Umeshaona Anavyokabwa Messi Uwanjani? Angalia Hapa

Sina haja ya kuongeza neno lolote zaidi ya kukuachia mwenyewe uangalie jinsi alivyozungukwa!!!!

Ronaldo Na Mourinho, Nani Muhimu Sana Kwa Madrid?

Cristiano Ronaldo na J ose Mourinho wanasemekana kuwa ni watu muhimu sana kwa yale wanayoyafanya. Ronaldo anaweza kuwa mchezaji bora wa mwaka na mara kwa mara huitwa mchezaji bora. Mourinho anafanana naye kwani hutajwa sana kama kocha bora wa soka. Ronaldo anaendelea kuvunja rekodi na anadhaniwa na wengi kwamba ni mchezaji bora wa soka duniani. Meneja wake tayari ameshashinda makombe ya Champions League na katika nchi mbalimbali ameshashinda makombe ya ligi. Kwa sasa watu hawa wawili wanaotazamwa na dunia wako kwenye timu moja ya Real Madrid , hivyo hufanya kutokea kwa swali- Nani ni muhimu zaidi ya mwenzake kwenye timu hiyo? Swala hili linaweza kuleta mabishano mengi kwa pande zote mbili, lakini pia linaweza kuleta wazo moja muhimu ya kwamba hakuna kilicho muhimu kwa Madrid zaidi ya mafanikio . Nayo ni kwamba kikosi kizima cha Madrid na wale wanaompa Mourinho nguvu wote wana wajibu wa kuleta mafanikio kama walivyo Ronaldo na Mourinho . Wewe mjadala wako ukoje juu ya wa

Jinsi Ilivyokuwa Kati Ya Madrid Na Barcelona Kwenye Super Cup

Real Madrid waliibuka na ushindi  wa magoli 2-1 dhidi ya Barcelona na  kufanya wafungane 4-4 (agg) na hivyo  Madrid kuwa mabingwa wa Super Cup  baada ya kuwa na magoli ya ugenini.  magoli ya Madrid yalifungwa na Gonzalo Higuain  na Cristiano Ronaldo, wakati lile la Barcelona  lilifungwa kwa Free-kick na Messi.  Huku Adriano akipewa kadi nyekundu baada  ya kumchezea Rafu Ronaldo aliyekuwa  akielekea kutingisha nyavu.   Gonzalo Higuain akishangilia goli baada ya kufunga  Messi akishangilia goli lake   Ronaldo naye akishangilia hapa  Ronaldo pamoja na Pepe wakilishikilia Kombe   Juu: Higuain akifunga goli wakati chini akishangilia kwa style ya kutereza chini  Ronaldo akifunga goli Picture Sources: MailOnline, GETTY IMAGES, Reuters, EPA

Torres Anauhakika Wa Kuziba Pengo La Drogba Chelsea

 Fernando Torres anauhakika kwamba ataziba pengo la Drogba kufuatia Mchazaji huyo toka Ivory Coast Kuuzwa huko Uchina kwenye timu ya Shanghai Shenhua. Drogba alijiunga na timu hiyo ya China baada ya kufunga magoli 157 kwenye timu yake ya Chelsea ndani ya miaka 8. Torres amesema yupo tayari kuiongoza Chelsea kwenye Champions League na kwamba anayapenda hayo majukumu na amekuwa akifanya hivyo maisha yake yote.   " Mahusiano yetu yalikuwa ni mazuri na nilikuwa naongea naye alipoamua kuondoka Chelsea, akanitakiwa mafanikio mazuri na kwamba huenda siku moja watu watanikumbuka mimi kama wanavyomkumbuka yeye ." Aliyasema Torres Julai 28 mwaka huu. Mpaka sasa tayari matunda ya juhudi zake yameanza kuonekana kwani ametokea kuwa ni mchezaji muhimu Chelsea kwa lengo lake la kufunga magoli.

Shanghai Shenhua Huenda Wakampoteza Drogba

Kibarua cha mchezaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba huenda kikafika kikomo kwenye timu yake mpya ya Shanghai Shenhua baada ya kutokea kwa mgogoro wa mapato kwa viongozi wa timu hiyo. Mwenyekiti wa timu hiyo Zhu Jun ametishia kuchomoa investment yake hivyo kuleta hisia kwamba Drogba na mwenzake Anelka Huenda wakauzwa. Zhu amekuwa akilipa mishahara ya pauni 200,000 kwa wachezaji hao kwa wiki na sasa ametishia kulipa asilimia 28.5 tu kama sehemu ya mchango wake kwenye timu. Zhu alitoa zaidi ya pauni milioni 60 kwenye timu kwa matarajio kwamba angepata faida ya asilimia 70, lakini jambo hilo limekuwa gumu sana na matokeo yake yupo tayari kuondoa investment yake kwenye timu hiyo.

Champions League Itakuwa Hivi..!!

CHAMPIONS LEAGUE GROUP STAGE DRAW SEEDING GROUP 1: Chelsea, Barcelona, Manchester United, Bayern Munich, Real Madrid, Arsenal, Porto, AC Milan. GROUP 2: Valencia, Benfica, Shakhtar Donetsk, Zenit St. Petersburg, Schalke, Manchester City, Braga, Dynamo Kiev. GROUP 3: Olympiacos, Ajax, Anderlecht, Juventus, Spartak Moscow, Paris Saint-Germain, Lille, Galatasaray. GROUP 4: Celtic, Borussia Dortmund, BATE Borisov, Dinamo Zagreb, CFR Cluj, Malaga, Montpellier, Nordsjaelland.   Source: Bloomberg News

Huyu Hapa Ni Usain Bolt

Usain Bolt amejizolea sifa kubwa  sana duniani baada ya kuonesha  umwamba wake wa mbio za mita  100 na 200 kwenye michezo ya  Olympic iliyofanyika mwezi uliopita  huko London Uingereza.  Mara zote alikuwa anatamba kwamba  atashinda  kabla ya mbio kufanyika  na wakati wa mbio ndicho alichofanya  na kusababisha watu wengi wa  mataifa mbalimbali kuvutiwa  naye na kumpenda sana.  Ilifikia hata watu wa mataifa mengine  walimshangilia kwa nguvu zote Imegundulika kwamba Usain Bolt  ni mshabiki mkubwa sana wa  Man United na anapokuwa  England hujaribu kuhudhuria  mechi zote za Mashetani hao wekundu. Kuna wakati alisikika akisema  kwamba anamwomba Sir Alex Ferguson  amsajili kwenye kikosi chake  kwani pamoja na kuwa na wachezaji  wenye vipaji pia timu inahitaji  wachezaji wenye mbio kama yeye.

Msimu wa Ligi Hispania: Nani zaidi Kati Ya Ronaldo na Messi.?

Tunaweza kuwaita ni wachezaji wa dunia kwani hata watoto wadogo wanawafahamu hawa zaidi kuliko wachezaji wengine wowote. Hiyo inatokana na ukweli usiofichika kwamba ni wachezaji muhimu sana kwenye timu zao na wanafanya yale ambayo timu na makocha wao wanatarajia na hivyo kuwafanya wabakie kwenye nafasi za juu ulimwenguni na kumzo kubwa. Messi na Ronaldo wakisalimiana     Wakati msimu wa ligi ya Hispania maarufu kama " Primera La Liga " ndiyo umeanza hivi karibuni, yameibuka maswali mengi sana miongoni mwa mashabiki wa Lionel Messi anayechezea Barcelona na wale wa Christiano Ronaldo anayechezea Real Madrid kwamba "nani atakuwa zaidi ya mwenzake msimu huu?."   Messi akifanya vitu vyake uwanjani Ronaldo huwa anaifunga Barcelona pale wanapokutana na Messi vivyo hivyo. Jambo ambalo linafanya swali la nani zaidi kuwa gumu sana kujibika kutokana na ukweli kwamba wote wawili ni wakali sana na kama mmoja anmzidi mwenzake basi ni kidogo sana. Y

Walcott Kwenda Man City?

Anaitwa Theo Walcot . Inasemekana Manchester City wanampango wa kutangaza dau la kumnunua mchezaji huyo baada ya kugundua kwamba anaweza asitie saini yake tena kuichezea Arsenal . Inasemekana Roberto Mancini anavutiwa sana na fowadi huyo wa Arsenal kwa muda mrefu sana kiasi kwamba huenda akatangaza dau ingawaje na Liverpool nao inaonekana wana lengo kama hilo. Mshauri wake alianzisha mazungumzo na Arsenal Ijumaa iliyopita ya kuhusu mkataba mwingine wa miaka mitano wa dola 75,000 kwa wiki, walakini wawakilishi wake inasemekana wanataka kuikataa ofa hiyo. Katika mazungumzo mengine ya Jamanne, Arsene Wenger akiwa anatamani kumbakiza winga wake huyo, yeye pamoja na uongozi wa club wamesema kwamba wanatarajia kumuuza mchezaji huyo kabla ya kufungwa kwa pazia la usajili Ijumaa kama hawatasikia chochote toka kwake kama anataraji kuendelea na Arsenal .

Unamfahamu Antonio Valencia? Huyu Hapa

  Valencia akiwa kwenye moja ya harakati zake za kuchonga krosi Alijiunga na Manchester United mwaka 2009 kwa donge la dola milioni 17. Naye ni raia wa Ecuador.  Ilikuwa ni wakati Christiano Ronaldo anahamia Real Madrid na kuacha pengo kubwa sana kwa Man United. Pengo ambalo hakuna aliyewahi kuwaza kwamba lingezibika. Lakini mara alipoanza kuichezea Man United alianza kuonesha kwamba anaweza kwani mbio pamoja na krosi zake kuelekea upande pinzani vilikuwa ni hatari tupu.  Alianza vizuri sana lakini akakumbwa na balaa la kuumia kiasi kwamba alikaa nje ya dimba kwa muda na kufanya watu washindwe kushuhudia uwezo wake vizuri. Msimu uliopita ndipo watu walipoona umuhimu wake na kipaji chake na kugundua kwamba ni winga wa kiwango cha juu sana. Akiwa na uwezo wa kukimbia na mpira kwenye wing ya kulia na kuachia mashuti yake  ya krosi kama risasi zikiwa zinawalenga Wayne Rooney pamoja na Javier Hernandez . Winga huyo ambaye watu hudhani ni old fashion, hapendi sana kupiga ch

Hivi Umesikia Shinji Kagawa Amesema Nini Kuhusu Sir Alex Ferguson?

Kagawa Asema: Sielewi chochote anachosema Ferguson . mchezaji huyo ndiyo kwanza anajaribu kujifunza Kiingereza na anakubali kuwa kwa kujaribu kutafsiri Kiingereza cha ki scotish cha kocha wake itamchukua muda sana kujipanga kwa maisha ya Uingereza.  Shinji Kagawa Kiungo wa Man United Shinji Kagawa aliyeshikwa kichwa  katikati ya Rafael na Van Persie

Barclays English Premier League: Hivi Ndivyo Ilivyokuwa

Manchester City Dhidi Ya Liverpool Hii ilikuwa ni Man City dhidi ya Liverpool. Ilikuwa ni moja ya mechi nzuri na kali sana tangu kuanza kwa English Premier League.  Liverpool walionekana kujipanga vizuri zaidi na kuwapa shida sana walinzi pamoja na viungo wa Man City.  Kama siyo makosa ya walinzi wa Liverpool ambao kwa namna moja au nyingine tunaweza kusema ndiyo waliochangia Man City kusawazisha magoli basi stori leo zingekuwa nyingine kabisa.  Magoli ya Man City yalifungwa na Yahya Toure na Carlos Tevez na yale ya Liverpool yalifungwa na Martin Skrtel pamoja na Suarez  Juu: Tevez alimpiga chenga kipa wa  Liverpool na kusawazisha goli la pili  kwa Man City baada ya mlinzi wa  Liverpool Martin Skrtel kufanya  makosa ya kurudisha mpira kwa  goli kipa bila kuangalia kama kuna adui ama la.  Juu: Hapa Tevez akishangilia baada ya  kufunga goli la pili kwa timu yake Juu:  Man City wakipongezana baada   ya kusawazisha goli la kwanza