Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2015

Wafwatao tayari wameanza Mbio za Urais ndani ya CCM

Mpaka Sasa wmeshajitokeza Mawaziri wawili na mbunge mmoja ndani ya CCM na kutangaza ni ya kugombea urais wa Tanzania huku wakisubiri ridhaa ya chama. Nao ni hawa:- 1. Mh Edward Ngoyai Lowasa ambaye ni mbunge wa Monduli na waziri mstaafu aliyetangaza nia jana 30/5/2015 jijini Arusha na kushuhudia umati mkubwa wa watu ukifulika kumsikiliza. 2. Stephen Wasira ambaye ni waziri wa kilimo ametangaza nia leo 31/5/2015 asubuhi katika ukumbi wa BOT jijini Mwanza. 3. Mwigulu Nchemba ambaye ni naibu waziri wa fedha anatangaza nia hivi Sasa katika ukumbi wa Mwl Nyerere katika Manispaa ya Dodoma yaliko makao makuu ya Serikali na CCM.

Lowasa Aweka Rekodi ya Umati wa Watu Sheikh Amri Abeid Arusha

Hatimaye Mh Edward Ngoyai Lowasa ametangaza kuwania urais kwa tikiti ya chama tawala cha CCM mbele ya umati wa wakazi wa jiji LA Arusha uliokusanyika kumsikiliza. Watu walianza kukusanyika uwanjani hapo mapema sana asubuhi wakisubiri mzee huyo kwa hamu kusikia akitangaza azma yake hiyo huku wakitumbuzwa kwa burudani nyingi toka kwa wasanii mbalimbali wa kitanzania. Unaweza kushuhudia mwenyewe kupitia picha hizo jinsi watanzania walivoitikia wito wake kufika uwanjani hapo wakiwemo waandishi wa Habari, wasanii mbalimbali, wachungaji, mashehe, maaskofu, manabii na mitume, viongozi mbalimbali wa CCM toka mikoa mingine akiwemo mwenyekiti wa CCM Geita anayejulikana kwa jina la MSUKUMA ambaye alitua uwanjani hapo kwa helikopta akitokea Geita. Wananchi walionesha kuvutiwa na kuipenda sana kauli aliyoitoa ya ''Maamuzi Magumu'' kwani kila alipotamka hivo tu umati ulipiga shangwe na mayowe kushangilia. Kauli ya pili iliyopendwa sana ni ili kauli mbiu yake ya mbio za urais inayo

Jinsi nilivombamba Mzee Magari kwenye Location na kupiganae picha

Ilikuwa Arusha Jana maeneo ya 88 Njiro, LA Mony Pub. muda ni usiku... Kidogo nami nitokee kwenye Muvi

Lowasa Kuhutubia Jiji la Arusha Leo. Ungana Nasi

Mkongwe wa siasa nchini Tanzania na aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Edward Lowasa anatarajiwa kuhutubia wananchi wa jiji la Arusha leo Jumamosi 30/05/2015 katika uwanja wa Sheik Amri Abeid. Mh Lowasa pia anatarajia kutangaza rasmi azma yake ya kuwania urais wa Tanzania. Usikose kurudi hapa baadae kupata habari zaidi.