Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2022

Spika Job Ndugai Abwaga Manyanga

SPIKA WA BUNGE LA JMT JOB NDUGAI AJIUZULU Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo Januari 06, 2022 ikiwa ni siku chache tangu kusambaa kwa video ambayo alinukuliwa akisema ipo siku Nchi itauzwa kutokana na madeni Amesema ameandika Barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM na uamuzi huo ni binafsi na hiari, na ameuchukua kwa kuzingatia maslahi mapana ya Nchi, Serikali na Chama.

Simba na Yanga Zagawa Dozi Mapinduzi Cup

Katika michezo iliyopigwa jana ya Mapinduzi Cup wababe wa soka Tanzania Simba na Yanga waligawa dozi muruwa na kuleta furaha na burudani kwa mashabiki wao. Simba wakicheza mchezo wao majira ya saa 10 jioni waliwabamiza Selem View fc kwa 2-0 huku magoli yao yakifungwa na Sakho pamoja na Bwalya.  Yanga wakikipiga milango ya saa 2 na robo usiku wakawafurumusha timu ya Taifa Jang'ombe kwa 2-0 huku magoli yao yakipigwa na Heritier Makambo (mzee wa kuwajaza) pamoja na Denis Nkane the wonder Kid aliyesajiliwa akitokea Biashara United.  Timu zote za Kariakoo Dar es Salaam zilicheza zikiwakosa nyota wao kadhaa ambao huwa wanaanza kwenye kikosi cha kwanza lakini bado zilisalia zikiwa mwiba vile vile. Je wewe umeonaje viwango vya Simba na Yanga bila baadhi ya nyota wao? Basi usiache ku comment ili tupate mawazo yako.