Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2019

€70 m + Gareth Bale + Toni Kroos = Paul Pogba

€70m + Gareth Bale + Toni Kroos = Paul Pogba Manchester United wanatarajiwa kupata kiasi cha pauni milioni 70 pamoja na wachezaji wawili, Gareth Bale na Toni Kroos kutoka Madrid endapo watakubari ofa hiyo kwa kumwachia Paul Pogba aende Barnabeu. (Daily Express) Manchester United will not only net a £70m transfer fee for Paul Pogba from Real Madrid but also get Gareth Bale and Toni Kroos in part-exchange. (Source: Daily Express)

Sadio Mane afunguka kuhusu kukosa penati. Aamua kuwaachia wengine wapige

Sadio Mane afunguka kuhusu kukosa penati Anasema, "Nimekosa penati kwenye mechi zote mbili na lazima nikubali kuwa sio uwiano mzuri. Sitaki kuiletea timu yangu matatizo na, angalao kwa kipindi hiki. Kwa sasa nitakaa mbali na hizi penati na kuwaachia wenzangi wapige."  Mimi nasema, he's very professional. Wewe unasemaje?  Senegal forward Sadio Mane: "I have missed penalties in both games and must admit that it is not a good ratio. "I do not want to penalise my team and, at least for the time being,  I'm going to stand aside for the penalties and let other team mates get  on with it."

Kumbe PSG hawataki kumuuza Neymar kwa Barcelona bali kwa Real Madrid

PSG HAWATAKI KUMUUZA NEYMAR KWA BARÇA BALI KWA REAL MADRID Club ya PSG ya Ufaransa haina lengo la kumuuza Neymar kwa Barcelona, timu ambayo wafaransa hao hawana mahusiano nayo mazuri. Kwa hiyo, kwa mujibu wa 'Marça', PSG wameona bora mbrazili Neymar ni bora auzwe kwa Real Madrid huku wakiwa wameshawatangazia ofa karibu mara mbili. Lakini jibu la Madrid linaonekana ni 'Hapana!' Madrid hawamtaki tena Neymar hata kama miezi kadhaa walionesha nia ya kuitaka saini yake. Neymar hatakiwi tena Barnabeu kwa sababu tayari wanaye Hazard, na pia wako na ndoto ya kumpata Mbappé. Kwa sasa Neymar atapaswa kusuniri PSG wamrahisishie kurudi Barcelona, maamuzi ambayo hayaonekani kuwa marahisi pamoja na namba 10 huyo na baba yake kuendelea kuwasumbua PSG ili aondoke.

Arjen Robben Astaafu Soka

Arjen Robben Astaafu Soka Baada ya kushinda kombe la ligi ya Ujerumani Bundesliga mara 8, winga Arjen Robben ametangaza kustaafu Soka.  Star huyo wa Bayern Munich na Uholanzi amefikia uamuzi huo akiwa na umri wa miaka 35.  Winga huyo amecheza soka lake kwa miaka 19, akiziwakilisha baadhi ya timu kubwa na maarufu ulaya kama PSV Eindhoven, Chelsea na Real Madrid kabla ya kutimkia Bayern Munich mwaka 2009. Amekaa na Bavarians kwa miaka 10 akishinda Bundesliga mara 8 na kufunga magoli 144 likiwemo la ushindi wao dhidi ya Borussia Dortmund kwenye fainali za ligi ya mabingwa ulaya.  Robben ameichezea timu yake ya taifa Uholanzi mechi 96 akifunga magoli 37.

UPENDO NI FARAJA

Simu yake iliita kwa sauti msikitini wakati wa swala, ilikuwa bahati mbaya. Imama alitoa khutba fupi ya mawaidha baada ya swala akimwelezea jamaa huyo kama mfano wa waumini wazembe. Waumini wengine walimlaumu baada ya swala kwa kuwasababishia usumbufu katika swala zao. Mkewe naye hakubaki nyuma, wakati wakirudi nyumbani aliendelea kumpa maneno kuhusu uzembe wake mpaka wanaingia nyumbani. Ndugu wengine walitikisa vichwa vyao kuonesha kukerwa sana na jambo alilolifanya. Alionekana kufedheheka, kuaibika na kudhalilika sana. Hilo lilijionesha usoni mwake. Hakukanyaga tena msikitini. Jioni ile alielekea Baa. Alionekana mwenye mhemko na kutetemeka. Alimwaga kinywaji chake mezani, chupa ilidondoka kwa bahati mbaya na kuwamwagikia baadhi ya watu. Wale waliomwagikiwa na kinywaji chake walimkimbilia. Alifumba macho akitrajia kuzabwa vibao au kuambiwa maneno makali. Badala yake walimuuliza kama ameumizwa na kipande cha chupa iliyovunjika. Mhudumu alimpa pole na kumpa tishu ajisafishe. Mfanyakazi