Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2015

Mgomo wa Madereva

Hatimaye waziri Gaudensia Kabaka ameingilia kati na kuwatangazia madereva waliokusanyika stand kuu ya ubungo kuwa hakutakuwa na haja ya wao kwenda kusoma tena kama ilivotangazwa awali na Mkuu wa chuo cha NIT ama Chuo cha Usafirishaji. Waziri aliongeza kusema kuwa amri iliyotangazwa na Mkuu wa chuo huyo haipo serikalini na wala haitambuliki na serikali na kuahidi kuwa suala hilo litajadiliwa na mawaziri wenzake kabla ya kutolewa taarifa yake. Madereva hao walionekana kufurahia sana kauli hiyo na kumuahidi kamanda Kova kuwa watakuwa tayari kufuata sheria huku akiwataka kurudia maneno yake mithili ya watu wanaoapishwa. Je, kitendo cha Mkuu wa chuo cha NIT kutoa kauli ya lazima kwa madereva kutakiwa kurudi chuoni kusoma, alikurupuka, ajui wajibu wake ama kujichukulia madaraka?