Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2020

WAGONJWA 37 WAPONA CORONA, 71 WASUBIRI VIPIMO VYA MWISHO

WAGONJWA 37 WAPONA CORONA, 71 WASUBIRI VIPIMO VYA MWISHO Wagonjwa 37 waliokuwa wameambukizwa virusi vya Corona #COVID19 wamepona na kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya vipimo vya mwisho kuthibitisha kwamba hawana maambukizi. “Watu hawa 108 hawana dalili zozote za ugonjwa kama vile homa au mwili kuchoka isipokuwa wapo katika vituo vya matibabu kusubiri vipimo vya mwisho ili kuthibika kwamba hawana virusi vya corona kabla ya kuruhusiwa kutoka vituoni,” amesema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. Waziri Ummy Mwalimu amewataka watu waliopona ugonjwa huo kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya ili kujikinga na maambukizi mapya ya COVID-19 kwani zipo tafiti zilizofanyika nchi mbalimbali ikiwamo China zimeonyesha kuwa watu wanaweza kupata maambukizi mapya kama asilimia 14. “Tunapenda kuwahimiza watu waliopona watoe elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) kwa jamii. Pia, Nitumie fursa hii kwa niaba ya Serikali kutoa shukrani

*GSM WAFANYA SURPRISE KWA WACHEZAJI WA YANGA*

*GSM WAFANYA SUPRISE KWA WACHEZAJI WA YANGA* Mdhamini wa Klabu ya Yanga leo alifanya Suprise ambayo wachezaji hawakuwa wameitarajia. Wachezaji wa Yanga waliitwa na Meneja wa Timu Abeid Mziba kuwa anaomba kukutana nao Mlimani City Bila kuwaambia anakusudia kufanya nini kwa wachezaji hao. Baada ya wachezaji kufika Mlimani City walipelekwa moja kwa moja kwenye Duka la GSM ndani ya Mlimani City na kukabidhiwa VOCHA YA SH. LAKI SITA KILA mchezaji na kutakiwa kutumia VOCHA hiyo kwenye maduka Ya GSM kwa kujipatia Bidhaa wanayoitaka. Wachezaji walifurahishwa sana na Jambo hilo. Nasasa GSM inakusudia kuwaalika wachezaji Waliooa kuwapeleka Wake zao kwa Suprise ambayo GSM hakuitanabahisha. Wachezaji ambao wapo nje ya Dar watakutana na Vocha zao wakirejea. Tazama picha Mbali mbali wakati wachezaji wa Yanga walipokuwa wakijipatia Mahitaji yao ndani ya Duka la GSM Mlimani City Leo 20/04/2020. @bigbros_tanzania_tv

Tundu Lisu amtaka Rais kurudi Ikulu

Tundu Lisu amtaka Rais kurudi Ikulu 'Mheshimiwa Rais Magufuli, Ikulu ya nchi yetu haiko Chato. Ikulu iko Dar es Salaam na Dodoma. Toka mafichoni Chato uje Ikulu kuongoza nchi dhidi ya corona. Ndivyo wanavyofanya viongozi wenzako dunia nzima. Usiwaachie Ummy na Majaliwa jukumu hilo. Wewe ndiye Rais, sio wao.'- Tundu Lissu @Tundulisu Chanzo: @kwanzatv

BREAKING NEWS: WAGONJWA WAPYA 84 WA CORONA TANZANIA

BREAKING NEWS: WAGONJWA WAPYA 84 WA CORONA TANZANIA Waziri Ummy Mwalimu ametangaza wagonjwa wapya 84 wa Corona nchini Tanzania, jumla wamefikia wagonjwa 254. DSM -33 Arusha -4 Mbeya -3 Kilimanjaro-3 Pwani -3 Tanga-3 Manyara-2 Tabora -1 Dodoma -3 Ruvuma -2 Moro- 2 Lindi-1 Mara-1 Mwanza -3 Mtwara -1 Kagera-1 Rukwa-2 Zanzibar-16 @eatv_tz

#COVID-19: TAARIFA KUTOKA BUNGENI, MBUNGE MMOJA AMEAMBUKIZWA CORONA

"Tumepata taarifa kuwa mmoja wetu amepata maambukizi ya #COVIDćƒ¼19. Mgonjwa huyo anaendelea vizuri na serikali inaendelea kumuangalia na kumpatia matibabu stahiki, na maelezo ya mbunge huyo alisafiri kwenda Dar es Salaam siku za hivi karibuni."- Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson @swahilitimes

PIERRE LIQUID ATHIBITIKA KUWA NA COVID-19

CORONAVIRUS-TANZANIA: PIERRE LIQUID ATHIBITIKA KUWA NA #COVID19 - Peter Mollel maarufu Pierre Liquid sasa yupo Hospitali ya Amana akiendelea na matibabu - Amesema anahisi amepata #CoronaVirus baa maana ndio maeneo yake ya kujidai @jforum #JFCOVID19_Updates

UFAFANUZI KIFO CHA EVODIA KAPINGA, MUUGUZI, MUHIMBILI

UFAFANUZI KIFO CHA EVODIA KAPINGA MUUGUZI, MUHIMBILI. Kuna taarifa inasambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Marehemu Evodia Kapinga amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Corona na kwamba alikua akihudumia wagonjwa wa Corona. Marehemu Kapinga hajawahi kuhudumia wagonjwa wa wanaougua ugonjwa wa Corona Marehemu alikua akitoa huduma kliniki ya watoto wenye tatizo la afya ya akili iliyopo jengo la watoto. Marehemu ni mgonjwa wa siku nyingi aliyekua akisumbuliwa na MARADHI AMBAYO HATUWEZI KUYATAJA KULINGANA NA MAADILI YA TIBA. Jana jumamosi tarehe 18 Aprili, 2020 saa NNE USIKU marehemu akiwa nyumbani kwake Kimara, alizidiwa ambapo watoto wake walifanya jitihada ya kumkimbiza Muhimbili lakini wakiwa njiani hali yake ilibadilika ndipo walipompeleka Hospitali ya karibu ya Sinza, Palestina. Madaktari na Wauguzi walifanya kila jitihada kuokoa maisha yake bila mafanikio ambapo amefariki leo jumapili saa 09 alfajiri. Hivyo, taarifa zinazosambaa kuwa kifo chake kinatokana na ugonjwa wa Corona siy

Vifo vya wagonjwa wa corona vyafikia 5

Wizara ya Afya Tanzania imesema vifo vya corona Tanzania vimeongezeka na kufikia vitano Kutoka vinne, pia kuna wagonjwa wapya 53 ambao wanafanya visa vya corona kufikia 147>>”DSM kuna wagonjwa wapya 38, Zanzibar (10), Mwanza (1),Kilimanjaro (1), Lindi (1),Pwani (1) na Kagera (1)” • “Hadi sasa tuna jumla ya Watu 147 waliopata maambukizi ya corona Tanzania, kati yao waliopona ni 11 na vifo 5, wagonjwa waliobaki (131) hali zao ni nzuri isipokuwa wanne ambao wanapatiwa matibabu ya wagonjwa mahututi kutokana na kusumbuliwa na matatizo mengine ya kiafya”- Waziri wa Afya Ummy Mwalimu  @ummymwalimu  #MillardAyoCORONATZ @millardayo

TANZANIA YATANGAZA WAGINJWA WAPYA 53 WA CORONA

TANZANIA YATANGAZA WAGONJWA WAPYA 53 WA CORONA Idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania yaongezeka nakufikia 147, baada ya wengine wapya 53 kukutwa na virusi vya Corona. Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema wagonjwa hao wote ni watanzania ambapo 38 ni kutoka Dar es Salaam,10 Zanzibar, Kilimanjaro 1,Mwanza 1,Pwani 1,Lindi 1,na Kagera 1. @azamtvtz

Dar: Makonda atoa wito wa kutosafiri bila sababu maalumu kuepuka corona virus

DAR: MAKONDA ATOA WITO WA KUTOSAFIRI BILA SABABU MAALUMU KUEPUKA #CORONAVIRUS > Amewaagiza Wenyeviti wa Mitaa kuzuia watu kukaa vijiweni ili kuepusha mirundikano na kuwachukulia hatua wale watakaokaidi maagizo hayo > Asema hali ya maambukizi ndani ya Mkoa sio nzuri hivyo kila mtu ajilinde #JF #JFCOVID19_Updates

Rais JPM Atangaza siku 3 za maombi kupambana na janga la corona

Amesema,  “Ndugu zangu Watanzania, kutokana na ugonjwa wa Corona, nawaomba tutumie siku 3 za kuanzia tarehe 16 - 18 Aprili, 2020 {Ijumaa, Jumamosi na Jumapili} kumuomba Mwenyezi Mungu aliye muweza wa yote atuepushe na janga la ugonjwa huu, tusali kila mmoja kwa imani yake, atatusikia”-JPM

Wizara ya Afya yathibitisha wagonjwa wengine 29 wa Corona

Wizara ya Afya Tanzania imesema kuna wagonjwa 29 waliothibitika kuwa na corona ambapo kati yao 26 wapo DSM, wawili Mwanza na mmoja yupo Kilimanjaro hivyo kufanya visa vya corona Tanzania kufikia 88, wagonjwa waliopona hadi leo ni 11 na vifo vya corona vimefikia vinne.

Idadi ya wagonjwa wa covid-19 Zanzibar yaongezeka

IDADI YA WAGONJWA WA COVID-19 ZANZIBAR YAONGEZEKA Wizara ya Afya Zanzibar imetoa taarifa ya kuongezeka kwa wagonjwa sita wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona na kufanya idadi ya wagonjwa kufikia 18 visiwani humo. Katika wagonjwa hao, watano ni raia wa Tanzania na mmoja raia wa Misri. #AzamTVUpdates #AzamNews #BreakingNews

Marekani yaweka rekodi mpya, waru 2,228 wafariki kwa covid-19 ndani ya saa 24

#CORONAVIRUS: MAREKANI YAWEKA REKODI MPYA, WATU 2,228 WAFARIKI NDANI YA SAA 24 > Idadi ya vifo imefikia 28,368 hadi sasa kwa mujibu wa Reuters > Pia, Nchi hiyo imerekodi Waathirika 606,194 wa #COVID19 hadi kufikia mapema leo #JFCOVID19_Updates #JamiiForum

"Serikali Isitangaze wagonjwa wapya wa corona": Mwigulu. Unaiongeleaje kauli yake hiyo?

Unaiongeleaje kauli ya Mwigulu Nchemba kwamba serikali isitangaze wagonjwa wapya wa covid-19? Tupe maoni yako tafadhali

SHULE, VYUO KUENDELEA KUFUNGWA, SHEREHE ZA MUUNGANO, MEI MOSI ZAAHIRISHWA

SHULE VYUO KUENDELEA KUFUNGWA, SHEREHE ZA MUUNGANO, MEI MOSI ZAAHIRISHWA Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema agizo la kufungwa kwa shule za awali, msingi, sekondari na vyuo vyote vya elimu ya kati na vya elimu ya juu litaendelea kubaki vile vile hadi hapo Serikali itakapotoa tamko jingine. Pia, Waziri Mkuu amesema Rais Magufuli amesitisha maadhimisho ya Sherehe za Muungano(Aprili 26) pamoja na Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ili kuepuka msongamano na kuendelea kuzuia virusi vya corona visisambae zaidi. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 14, 2020) katika kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano Dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Mapafu unaotokana na maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID-19). Amesema hadi leo, nchini kuna jumla ya watu 53 waliobainika kuwa na virusi vya corona ikiwa ni ongezeko la wagonjwa wanne ambao wote wapo jijini Dar es Salaam. Amesema Serikali bado haijatangaza kuhusu kufunguliwa kwa shule, vyuo na shughuli za michezo pamoja na misongamano i

Ali Kiba Afunguka baada ya wasanii wake wawili kuondoka kwenye lebo yake ya Kings Music

Unapomtendea mtu jambo lake tena kwa mapenzi yote  Usitarajie fadhira wala malipo baadae Kwasababu kuna aina nyingi ya binaadam  Sio Kila mmoja ana MOYO kama wako.  Ali Kiba

Milioni 500 za Muungano kupambana na covid-19

"Shilingi milioni 500 ambazo zilitengwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 56 ya Sherehe za Muungano zipelekwe kwenye mfuko wa kupambana na COVID-19 wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar"-Rais Dkt. Magufuli #ITVTanzania

Simba sc waingiza sh milioni 130 kila mwezi kutoka kwa Mo Dewji

Simba sc waingiza sh milioni 130 kila mwezi kutoka kwa mwekezaji wao Mo Dewji OFISA Habari wa Simba, Haji Sunday Manara amesema kuwa Simba inaingiza fedha zaidi ya Sh milioni 130 kila mwezi kama gawiwo kutoka kwenye fedha ya mwekezaji. Fedha inayotakiwa kutolewa na mwekezaji ni Sh bilioni 20 ili amiliki sehemu ya 49% ya klabu hiyo na Manara amesema fedha hizo kama walivyokubaliana zimeingizwa benki ambako watakuwa wakipata gawio ambalo tayari wameanza kulipata kwa kuchukua zaidi ya sh milioni 130 kila mwezi. “Simba ishaanza kupokea sehemu ya gawio au ziada lakini kuna fedha tunapata kutoka katika fixed account. Mfano ukiweka milioni 100 kuna kiasi fulani unapata, sasa kwa fedha iliyowekwa sisi tunapata na inatusaidia katika masuala ya mishahara. “Sisi niseme nia ya mabadiliko ipo na kubwa sasa Simba  inakula fedha ya gawio kutoka katika fedha tuliyokubaliana iwekwe kama sehemu ya manunuzi ya Simba,” anasema Manara. “Nimesikia hili limeibuliwa na haya ndiyo majibu yake na huenda wengi h

Wagonjwa wa corona waongezeka Tanzania

Wagonjwa wa corona waongezeka Tanzania Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu ametangaza ongezeko la wagonjwa wengine wapya 14 wa virusi vya Corona nchini. Wagonjwa hao wote ni Watanzania, kati yao 13 wako Dar es Salaam na mmoja wa Arusha. #ITVTanzania

According to your opinion, who is better than the other, Ronaldo De Lima from Brazil or Cristiano Ronaldo from Portugal?

Who is better?

MSHINDI WA BONGO STAR SEARCH HAJALIPWA HELA YAKE, NAIBU WAZIRI AINGILIA KATI

Naibu Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mhe.Juliana Shonza ametoa mwezi mmoja kwa uongozi wa Kampuni ya Benchmark Production inayoendesha mashindano ya kusaka vipaji kwa wasanii wa muziki maarufu kama Bongo Star Search (BSS) kuhakikisha wamemlipa mshindi wa kwanza wa mwaka 2019 zawadi yake ya Shilingi Milioni 50. #ViwanjaniLeo

Mama wa Kocha Pep Guardiola Afariki kwa Corona virus

Mama wa ‪Pep Guardiola, Dolors Sala CarriĆ³ amefariki dunia kufwatia maambukizi ya coronavirus, club imethibitisha. Alikuwa na umri wa miaka 82.‬ ‪Mungu aipokee roho ya marehemu. ‪(Source: Manchester City)

Updates ya Corona Duniani

Vifo kutokana na corona Marekani vimefikia 5149 mchana huu, kwa takwimu hizi Marekani imeendelea kuizidi China ambayo ina idadi ileile iliyoripotiwa jana ya vifo 3312, Marekani pia inaongoza kwa wagonjwa wa corona Duniani ambapo leo wamefikia 216,761, China ina wagonjwa 81,589. • Jumla ya vifo kutokana na corona Duniani kote mchana huu imefikia Watu 47,364 huku wagonjwa wakifikia 937,560 na waliopona ni 196,529. Chanzo: #MillardAyoUPDATES