Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2017

Paul Pogba amwambia Mourinho: Sitaki kupumzishwa!

Kiungo wa Manchester United Paul Labile Pogba amemsihi meneja wake Jose Mourinho asimpumzishe kwa sababu ya kuhifia kwamba bado hayuko fit kimchezo ama kuhofia kwamba atamchosha. Pogba ambaye ametoka kupata nafuu ama kupona kutokana na majeraha aliyoyapata zaidi ya miezi miwili aliliambia gazeti la Manchester Evening News kuwa kuelekea mechi na Arsenal ni lazima apate nafasi ya kucheza muda wa kutosha kwani amekuwa mwanasoka kwa sababu hiyo na pia anafurahia kucheza.  Mourinho hatakuwa na budi kumchezesha Pogba muda wa kutosha ukizingatia kutokuwa fit kwa Nemanja Matic na Fellaini. Na Pogba ambaye ameahacheza dakika 90 katika mechi 2 amekuwa mhimili mkubwa kwenye kikosi cha United katika eneo lake la kiungo! Akuleta ari kubwa ya mchezo kwa wenzake. Kikosi cha Manchester United kitasafiri kwenye Emirates kukwaana na Arsenal siku ya Jumamosi katika kampeni za kuwania ubingwa wa Ligi ya Uingereza. Kikosi hicho kilicho chini ya Jose Mourinho kipo Katika nafasi ya pili nyuma ya Mancheste

Lowassa awaambia wananchi kuwa hana haja wala ndoto za kurudi CCM

Akiwa katika kampeni za Kumnadi mgombea wa udiwani kata ya Makabi wilayani Meru,  waziri mstaafu na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA,  Edward Lowassa alijibu hija zilizokuwa zikienea kwamba ana mpango wa kurudi CCM.  Amesema kuwa taarifa zozote zinazodai hivyo ni za uzushi na zina lengo la kupotosha. Muungwana Blog iliandika kuwa kuna habari zilizoenea kuwa Mrisho Gambo amepokea ujumbe toka kwa mzee wa Monduli uliomtaka kuzungumza na Rais na kama atakubali basi mzee huyo atarejea nyumbani.  Lakini mzee Lowassa amezikana habari hizo na kusema kuwa ni upotoshaji na kwamba yeye hana nia wala ndoto za kurejea CCM.

Hatimaye David Kafulila akabidhiwa rasmi kadi ya uwanachama wa CCM

Zikiwa zimepita siku tatu tu tangu David Kafulila ahame CHADEMA,  Leo amekabidhiwa rasmi kadi ya uwanachama wa CCM na Humphrey Polepole wakati wa kampeni za udiwani kata ya Mbweni jijini Dar es Salaam.  Bwana David Kafulila alitangaza rasmi kuhama CHADEMA siku ya Jumatano kwa madai kwamba upinzani hauna nia ya kupambana dhidi ya ufisadi. Kitendo cha Kafulila kuhama CHADEMA kumeleta gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki wa siasa nchini huku swala hilo likienda mbali zaidi na kugusa hata yao hasa pale ilipofahamika kwa mume amehamia CCM na kumwacha Mke CHADEMA akiwa mbunge wa viti maalumu.  Kituko zaidi ni pale Mke aliposikika akidai kuwa mume wake atoe Sababu za msingi za kuhama chama na kwamba hakumshirikisha maamuzi hayo.  Naye Kafulila alisikika akidai kuwa swala la yeye kuhama chama halina mahusiano yoyote na ndoa yake.

Jacqueline Wolper awajia juu mastaa wenzake wasiochangia biashara yake

Staa wa bongo movie Jacqueline Wolper amefunguka kwa kusema kuwa tangu ameanzisha biashara yake ya ushonaji anapata wateja mbalimbali ambao ni wa kawaida na kuwa ni ngumu sana kupata mastaa wenzake badala yake anaowapata hawazidi hata watatu. Kwa mujibu wa #MuungwanaBlog,  Wolper amedai kuwa pale mtu anapoanzisha biashara wengine hawapendelei badala yake hununa na kugoma kutoa ushiriano au support. Jamani wana bongo movie mnashindwaje kumuunga mkono mwenzenu?  Au mnataka akale polisi?  Sio fresh hivyo.  Acheni hizo.

MANGE AMTAKA MKE WA DAVID KAFULILA KUOMBA TALAKA

MANGE AMTAKA MKE WA DAVID KAFULILA KUOMBA TALAKA Mange Kimambi ameibuka na kumtaka mke wa mwanasiasa maarufu nchini David Kafulila kudai talaka kwa sababu ya kitendo cha mumewe kuhama chama cha CHADEMA. Kwa mujibu wa mke wa Kafulila, mumewe alihama chama bila kumshirikisha kama mke wake na kuwa sababu alizozitaja za kumfanya ahame hazina mashing.  Hivyo Mange Kimambi amemwomba kama kweli yuko serious na hilo basi adai talaka ama la itakuwa ni mambo ambayo wameshirikiana kupanga ili wale kotekote. Yaani mke apate mshiko CHADEMA ambako yeye ni mbunge wa viti maalum kupitia chama hicho kinara cha upinzani na mumewe ale CCM alikohamia.  Pia Mange aliendelea na swaga hilo kwa kumshauri kuwa pindi atakapodai talaka  asisahau na kudai matunzo ya mtoto wazungu wanaita "child support" Kwani mumewe kwa sasa ana hela kinyama.  Na kwamba yeye bado ni mrembo hatakosa mtu.  Hehe he. Mh haya bhana.  Msomaji sijui imekaaje hii mtu wangu wa nguvu? 👀👀

PSG wafanya karamu ya magoli kwa kuwachapa Celtic 7-1

PSG walifanya karamu ya magoli Jana Usiku kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwawasha Celtic kwa 7-1 katika mchezo wa kundi B.  Walikuwa ni Celtic walioanza kuliona lango na kuwafanya PSG wachachamae kutafuta kusawazisha na hatimaye ushindi na yaliyotokea ndio hayo.  PSG wameweka rekodi ya kufunga magoli mengi kwenye hatua ya makundi ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Chelsea wagawa kichapo cha 4G Kwa Karabag

Magoli mawili ya Willian na penati mbili za Hazard na Fabregas vilitosha Kabisa kuwazamisha vijana machachari wa Karabag ambao walionekana kuuanza mchezo vizuri sana lakini ubora na umakini wa Chelsea uliwafanya kupotea na kujikuta ikikaribisha kichapo hicho cha 4 bila kilichowawezesha vijana wa Antonio Conte kutinga katika hatua ya 16 bora kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Michael Lang aizamisha Manchester United

Wakicheza Katika performance ya juu ya umiliki wa mpira ukiwa 74% kwa 26%,  70% kwa 30% na 72% kwa 28%,  Manchester United walishindwa Kabisa kuchungulia nyavu za Basel Katika mchezo wa ligi ya Mabingwa ama champions League ya ulaya. Mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Basel 0, Manchester United 0. Lakini mambo yakabadilika kwenye kipindi cha pili katika dakika ya 89 pale mid field ilipozubaa kidogo na kusababisha Michael Lang kupokea krosi aliyoizamisha nyavuni na kumwacha kipa Romero asijue cha kufanya. Bado Manchester United wanashikilia usukani katika kundi lao wakiwa na pointi12 ambazo zinaweza kufikiwa na CSKA Moskva endapo watawafunga Manchester United magoli kuanzia 7 pale watakapokutana kwenye mechi yao ya mwisho ya kundi lao ili waweze kuibuka vinara wa kundi hilo

Kama ulipitwa na tukio la Kujiuzulu kwa Robert Mugabe aliyekuwa rais wa Zimbabwe, fungua hapa kuiona barua ya kujiuzulu aliyoiandika

Godbless Lema afunguka juu ya David Kafulila kuhama CHADEMA

Mbunge was Arusha mjini Mh Godbless Lema afunguka na kuzungumza juu ya kitendo cha David Kafulila kuhama chama cha CHADEMA. Amesema kuwa upo uwezekano mkubwa wa kumshauri na mke wake ambaye ni mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA kufanya kama alivyofanya yeye.  David Kafulila alitangaza leo kuhama chama cha CHADEMA kwa madai kuwa vyama vya upinzani havina nia thabiti ya kupambana na ufisadi.  Je,  ni kweli kuwa vyama vya upinzani havina nia thabiti ya kupambana na ufisadi?  Toa maoni yako! 

Ungependa kujua striker gani atatua Old Trafford hapo Januari 2018? Basi ingia hapa kumcheki

Zipo fununu kuwa meneja wa Manchester United anataka kuimarisha kikosi chake kwenye safu ya ushambuliaji kwa kumwinda striker kutoka Atletico Madrid ya Uhispania. Mitandao mbalimbali ulaya imeanza kuandika fununu za uhamisho maarufu kama usajili wa dirisha dogo la Januari huku anayetajwa sana kujiunga na United si mwingine bali Antoine Griezmann wa Atletico Madrid. Akihojiwa juu ya tetesi hizo mwenyewe Griezmann amesema kuwa bado ana mkataba mrefu na timu yake ya Atletico Madrid lakini hilo haliwezi pia kumzuia kuondoka huku akidai anataka kumalizia soka lake Marekani kama alivyofanya David Beckham ambaye alikuwa akimtukuza sana. Griezmann aliendelea kusema kuwa uwezekano wa kutimkia Uingereza hasa Manchester United upo isipokuwa kikwazo kikubwa ni hali ya hewa ya huko. Je,  Manchester United watafanikiwa kusajili Griezmann kwenye kipindi cha usajili wa dirisha dogo hapo Januari 2018?

Jengo la kituo cha habari cha Clouds Media laungua moto. Tazama picha jeshi la zimamoto wakiudhibiti moto huo

CLOUDS MEDIA TANZANIA: Jeshi la zima moto limefika katika jengo la kituo cha habari cha Clouds  Media Group mjini Dar es salaam kudhibiti moto uliozuka katika mojawapo ya vyumba vya kurushia matangazo ya televisheni. Chanzo cha moto hadi sasa bado hakijafahamika.Tayari moto umeshadhbitiwa. Hamna majeruhi wala vifo na thamani ya uharibifu haijafahamika bado #abelrk.blogspot.com

Habari za football zilizovuma leo majuu ni hizi hapa

Unataka kujua Neymar Jr na Marcus Rashford walikuwa wanazungumza nini siku wamekutana kwenye mechi ya England vs Brazil? Check hapa

Cristiano Ronaldo to quit Bernabeu?

Ronaldo delivers Real bombshell: An 'angry' Cristiano Ronaldo has reportedly rejected a new contract at Real Madrid and demanded a transfer away from the Spanish giants at the end of the season. Ronaldo, who has previously made it clear he didn't want to extend his current deal which runs out in 2021, was believed to have wanted to quit the club last summer. The Portuguese superstar opted to remain at the Bernabeu but reports in Spain on Tuesday have now suggested he doesn't want to play for the club beyond this term.

Waziri Mstaafu Lazaro Nyalandu aendelea kutoa ya moyoni kwa jamii

BAADA ya kutenda mema, wakasema ASULUBIWE! Na LazaroNyalandu NIMEINGIA Wizara ya Maliasili na Utalii kwa uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete, Mnamo Februari 10, 2014, na nimefanya kazi ya Uwaziri kwa takribani miezi 18. Itakubukwa kwamba kipindi hiki kilikuwa ni kilele cha ujangili wa Tembo barani Afrika, huku Tanzania ikitajwa kuwa nchi kinara kwa masuala ya ujangili wa wanyamapori, hususani Tembo. Wakati huo, akiba ya meno ya Tembo katika Ghala la Taifa yalifikia takribani tani 130,000, ikiwa ni idadi kubwa ya meno ya Tembo yaliyohifadhiwa popote duniani. Kazi yangu ya kwanza ilikuwa ni kuongozana na Rais Jakaya Kikwete kwenda London, Uingereza kuhudhuria Mkutano wa Tembo duniani ulioandaliwa na Mwana Mfalme Charles wa Uingereza, ambako pamoja na mambo mengine, Rais Jakaya Kikwete aliitaarifu dunia juu ya uamuzi wa Tanzania wa kupiga marufuku biashara ya meno ya Tembo, na kuungana na Mataifa lukuki yaliyokubali kufanya hivyo. Aidha, kwa kushirikiana na Rais Jakaya Kikwete, tulikubali T

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe awekwa kizuizini na jeshi la nchi hiyo

MUGABE KIZUIZINI: Jeshi la Zimbabwe lathibitisha kumweka kizuizini rais Robert Mugabe na mkewe, na kwamba kwa sasa limechukua udhibiti wa ofisi za serikali na kuweka doria katika mitaa ya mji mkuu wa Harare.

Lawrence Masha Aikacha CHADEMA! Kisa? Fungua usome!

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha atangaza kujivua Uanachama wa CHADEMA kwa madai kuwa viongozi wa chama hicho hawana nia ya dhati ya kuunda serikali na kushika dola. - JamiiForums imefanya jitihada za kuwasiliana na CHADEMA ambapo wamekiri kuondoka kwa Masha na wamesema watatoa tamko baadae kuhusiana na hilo.

BREAKING NEWS: Mume wa zamani wa Irene Uwoya Ndikumana Katauti amefariki dunia

Mume wa zamani wa Mwigizaji Irene Uwoya, Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda, Ndikumana Katauti (39) amefariki ambapo chanzo cha kifo chake bado hakijatajwa.

Aliyoyaandika Mh Lazaro Nyalandu katika ukurasa wake wa Facebook baada ya Kigwangala kumtuhumu Bungeni

INASIKITISHA sana kuona WAZIRI Kigwangalla akitumia MUDA wake ndani ya BUNGE leo kunichafua, kunidhihaki, na kusema UONGO na UZUSHI dhidi yangu, ikiwa ni NJAMA za makusudi zilizopangwa kunichafua mara baada ya mimi kukihama Chama Cha Mapinduzi -CCM. Aidha, hatua hiyo imepangwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa hakuna kiongozi yeyote wa CCM atakayethubutu ama kudiriki tena kukihama Chama Cha Mapinduzi CCM katika Serikali hii ya awali ya tano. AIDHA, Waziri Kigwangalla anatumika VIBAYA, kwa u za UONGO na UZUSHI aliuanza DHIDI yangu mara tu alipoteuliwa, kwa kuanza kutoa kauli za kejeli dhidi ya UTUMISHI wangu uliotukuka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii na wenye REKODI thabiti. NIANZE na UZUSHI alioutoa Waziri Kigwangalla  mapema leo BUNGENI, huku moyoni mwake akiwa anajua fika kuwa ametumwa kusema UONGO dhidi ya Waziri Nyalandu kwa lengo la kuandaa MAZINGIRA ya kumkamata na kubwa zaidi, kudhalilisha azma ya WATANZANIA ambao WAKO tayari kwa mabadiliko ya UONGOZI wa nchi kupitia UPINZAN