Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2020

RAIS MAGUFULI: UGONJWA USIWE SABABU YA KURUDI NYUMA.

RAIS MAGUFULI: KAMWE UGONJWA HUU USIWE SABABU YA KURUDI NYUMA “Ndugu Wafanyakazi wenzangu nawapongeza sana kwa kuchapa kazi, mimi nipo pamoja nanyi na natambua kazi nzuri mnayoifanya, nawaomba katika kipindi hiki ambacho dunia inapita katika wakati mgumu wa kukabiliana na ugonjwa wa #Corona, sisi tuendelee kuchapakazi, kamwe ugonjwa huu usiwe sababu ya kurudi nyuma na kuacha kuwahudumia Watanzania, mimi naamini Mwenyezi Mungu atatuvusha, ” - Rais Magufuli. #RaisMagufuli amewapongeza na kuwatakia heri wafanyakazi wote hapa nchini ambao leo tarehe 01 Mei, 2020 wanaadhimisha siku ya wafanyakazi #MeiMosi. Mwaka huu sherehe za Mei Mosi hazitafanyika ili kuepusha mikusanyiko ya watu, ikiwa ni hatua muhimu ya kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19). # MwenyeziMunguAtuvusha #Covid19 #CoronaTanzania #CoronaDeaths #VifoCorona Credit: #AZAMTV

Rais Dk. John P. Magufuli atangaza kifo cha Balozi Dk. augustine Mahiga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli anatangaza kifo cha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Balozi Dkt Augustine Philip Mahiga (Mbunge) kilichotokea leo Alfajiri tarehe 01 Mei, 2020.. Mhe.Balozi Mahiga ameugua ghafla akiwa nyumbani kwake. #ITVTanzania