Picha mbilli za Alfan Mrisho Ngassa
Yule mshambuliaji wa Azam FC na Taifa Stars, Alfan Mrisho Ngassa amejiunga na timu ya Simba kwa donge la shilingi milioni 25, ukweli umethibitika.
Azam wamethibitisha hilo na kusema kuwa mchezaji huyo ameuzwa Simba na ataanza kuichezea timu hiyo kwenye msimu ujao wa ligi na kwamba sasa Simba wanayo haki ya kumuita mchezaji wao, alithibitisha Patrick Kahemele, Meneja wa Azam.
Hapo awali Azam walisema kuwa Simba walikua mstari a mbele kumuwania Ngassa aliyeenda Azam akitokea Yanga kwa kuvunja rekodi ya uhamisho Tanzania misimu miwili iliyopita.
Wakati wa michuano ya cecafa Kagame Cup, Azam walionesha nia ya kumuuza mchezaji huyo baada ya yeye kuonesha hadharani kutokuwa na mapenzi tena na timu hiyo kwa kuibusu nembo ya timu ya Yanga.
Yanga pia walikuwa kwenye mbio za kumuwania mwana ndinga huyo lakini walitoa ofa ya shilingi milioni 20 tu na kukataa kuongeza dau, kitu ambacho kiliiweka Simba kwenye nafasi nzuri ya kumnyakuwa Ngassa.
Website ya Azam ilisema kwamba, "Tulipenda sana kumuuza Ngassa kwa Yanga lakini hawakutaka kutoa ofa nzuri."
Ngassa alijiunga na Azam mwaka 2010 kwa mshiko wa dola za marekani 40,000, pesa ambayo ilivunja rekodi za uhamisho kwa soka la Tanzania.
Alishawahi kwenda kufanya majaribio na timu ya Seatle Sounder FC na aliingia kama sub siku timu hiyo ilipokipiga na Man United kwenye mechi yao ya kirafiki.
Comments