UEFA CHAMPIONS LEAGUE🏆🏆🏆
Mipambano miwili iliyopigwa usiku huu ya UEFA Champions League imemalizika kwa matokeo ambayo wengi hawakuyatarajia lakini ndio mpira ulivyo.
Liverpool vs Manchester City
Liverpool wamewaadabisha vilivyo Manchester city kwa kuwapa kipigo kitakatifu cha magoli 3-0 magoli ambayo yalipatikana katika kipindi cha kwanza ndani ya dakika 30 za mwanzo yakifungwa na Mohamed Salah, Chamberlain na Sadio Mané.
Katika mchezo huo ambao Pep Guardiola ameshangazwa kwa kichapo imeshuhudiwa Mohamed Salah akiumia na hivyo kuleta hofu kwa ushiriki wake kwenye michezo ya city ya hivi karibuni.
Barcelona vs Roma
Barcelona wamewagalagaza Roma kutoka Italy kwa kichapo cha magoli 4-1 katika mchezo mwingine wa UEFA champions League.
Roma walionekana kuwa na tension ambayo ilisababisha wajifunge mara mbili na Barcelona wenyewe wakaongeza mengine mawili na kufanya waibuke na ushindi wa 4-1.
Comments