Skip to main content

Simba na Yanga Zagawa Dozi Mapinduzi Cup

Katika michezo iliyopigwa jana ya Mapinduzi Cup wababe wa soka Tanzania Simba na Yanga waligawa dozi muruwa na kuleta furaha na burudani kwa mashabiki wao.

Simba wakicheza mchezo wao majira ya saa 10 jioni waliwabamiza Selem View fc kwa 2-0 huku magoli yao yakifungwa na Sakho pamoja na Bwalya. 

Yanga wakikipiga milango ya saa 2 na robo usiku wakawafurumusha timu ya Taifa Jang'ombe kwa 2-0 huku magoli yao yakipigwa na Heritier Makambo (mzee wa kuwajaza) pamoja na Denis Nkane the wonder Kid aliyesajiliwa akitokea Biashara United. 

Timu zote za Kariakoo Dar es Salaam zilicheza zikiwakosa nyota wao kadhaa ambao huwa wanaanza kwenye kikosi cha kwanza lakini bado zilisalia zikiwa mwiba vile vile.

Je wewe umeonaje viwango vya Simba na Yanga bila baadhi ya nyota wao? Basi usiache ku comment ili tupate mawazo yako.



Comments

Popular posts from this blog

Joti naye auaga ukapera

Msanii wa maigizo ya vichekesho nchini maarufu kama Joti nae ameliaga kundi la makapera baada ya kufunga ndoa. Msanii Joti pia ni maarufu sana katika matangazo ya mtandao wa Tigo. Joti pia ni maarufu sana katika kuigiza sehemu mbalimbali kwani mara nyingi huigiza kama kijana wa kawaida, babu, mtoto na wakati mwingine huigiza kama msichana. Hongera sana Joti kwa kuoa! May your marriage last forever!

Ni Sawa Kwa Man City Kumuuza Mario Balotelli?

Ni mchezaji mwenye purukushani za kutosha awapo uwanjani. Purukushani zake ni za aina mbili. Zipo zile zinazoisaidia timu yake ya Man City pamoja na timu yake ya taifa ya Italy. Lakini pia zipo zile zinazowafanya siyo washabiki wa soka tu wakereke bali pia hata makocha wake. Lakini Balotelli ni mchezaji mwenye kipaji cha cha pekee kwa miongoni mwa wachezaji wa umri wake. Lakini sports director wa Man City, Brian Marwood, alikuwa na haya ya kusema kumuhusu Balotelli.   “I think that it’s important to make a good example. I think – and we all know who we are talking about – that you will get people within the system who do not show the right values and the right behavior. “In the main, we have a ­fantastic group of players here. I look at Pablo Zabaleta , I look at Vincent Kompany , I look at Joe Hart, Gareth Barry and Joleon Lescott. “I think we have a lot of players who can behave in the right way. You just have to make sure that they are the role models.” Katika ma